KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

comments
Kati ya Kuku na Yai Kipi Kilianza?

Mjadala wa miaka mingi kuhusiana na kipi kilitokea mwanzo kuku au yai? umepata jibu baada ya wanasayansi kuthibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo awali kabla ya yai.Mjadala wa miaka nenda rudi kuwa kuku na yai kipi kilitangulia duniani umepatiwa jibu na wanasayansi wa nchini Uingereza ambao wamethibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo mwanzo kabla ya yai.

Kwa kuangalia jinsi ganda la yai lilivyotokea, wanasayansi wa nchini Uingereza wanaamini wamepata jibu la mjadala huo.

Watafiti katika vyuo vikuu vya Sheffield na Warwick nchini Uingereza wamegundua kuwa protini inayoitwa ovocleidin (OC-17) ni muhimu sana katika kutengenezwa kwa gamba la yai.

Lakini protini hiyo hupatikana toka kwenye ovari ya kuku mwenye ujauzito.

Kwa maana hiyo yai lisingekuwepo kama kusingekuwa na protini ambayo inatoka kwa kuku mjamzito.

Watafiti hao waliongeza kuwa protini ya OC-17 husababisha calcium carbonate kwenye mwili wa kuku ibadilike kuwa calcite crystals ambazo ndizo hulifanya gamba gumu la yai ambalo hukilinda kiini cha yai wakati kuku anapoanza kukua ndani ya yai.

Hata hivyo wanasayansi wengine bado hawajaridhika na jibu lililotolewa kuwa kuku ndiye aliyetangulia kabla ya yai.Chanzo:Nifahamishe


TAHADHARI UKIWEKA LAPTOP MAPAJANI ZINAUA NGUVU ZA KIUME NA KUHARIBU MBEGU ZA KIUME

comments
Scott Reed aliathirika kwa kuweka Laptop Mapajani
I
Imethibitishwa kitaalamu kuwa joto linalotolewa na laptop inapotumika ikiwa mapajani hupelekea kuharibika kwa mbegu za kiume na kuwafanya wanaume washindwe kupata watoto na wapenzi wao.

 Scott Reed alifikiria kwenda na mkewe hospitali kujaribu njia ya kupandikiza mimba baada ya kuhangaika muda mrefu kujaribu kupata mtoto bila mafanikio.

Kitu ambacho Scott hakuweza kukifikiria ni pale alipoambiwa na madaktari kuwa laptop yake anayoitumia mara kwa mara akiwa ameiweka mapajani ndio chanzo cha tatizo lake la kutopata mtoto.

Madaktari walimuambia kuwa joto linalotokana na laptop yake inapotumika ikiwa mapajani husababisha kuharibika kwa mbegu za kiume na hivyo kumfanya ashindwe kupata mtoto.

Scott mwenye umri wa miaka 30 aliamua kuanza kuitumia laptop yake akiwa ameiweka kwenye meza na matunda yake yalijionyesha baada ya miezi mitatu ambapo mkewe Laura ambaye naye ana umri wa miaka 30 alipopata ujauzito.

Hivi sasa ikiwa ni miezi 10 baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa kike Taryn, Scott na mkewe ambao wanaishi kwenye mji wa Clanfield, Hants, bado hawaamini jibu la tatizo lao kuwa lilikuwa ni laptop.

"Sikuwahi kusikia kuhusiana na laptop kuharibu mbegu za kiume, nilishtuka sana", alisema Laura.

"Scott alikuwa akiitumia laptop yake kila siku jioni kwa masaa kadhaa akiwa ameiweka mapajani huku tukiangalia TV, hatukuwahi kufikiria kuwa ilikuwa na madhara na ilikuwa ikiharibu mbegu zake za kiume", aliongeza Laura.

Naye daktari bingwa wa masuala ya uzazi Sue Kenworthy alithibitisha madhara ya laptop kwa kusema kuwa wanaume inabidi watumie laptop wakiwa wameiweka kwenye meza badala ya kuiweka mapajani.

Chanzo: Nifahamishe

CHAMA CHA WANAHABARI WANAWAKE (TAMWA) KUTOA MAFUNZO YA UKATILI WA KIJINSIA KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA

comments

Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) Kinatarajia kuendesha mafunzo kwa Waandishi wa habari Mkoani Mara ili waweze kuibua na kuandika habari za Ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi Mtendaji wa chama hicho Valerie Msoka mafunzo hayo yanalenga kuadhimisha siku 16 za kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia na lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa Habari  kuripoto swala la ukeketaji na kuandika habari zaidi kuhusu swala hilo.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa Mkoa wa Mara ndio unaongoza kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ukifuatiwa na mkoa wa dodoma.

Waandishi wa habari Mara kupitia chama cha waandishi wa habari mkoa (MRPC) Wanatarajia kushiriki mafunzo hayo kikamilifu ili waweze kuibua na kuripoti habari za ukatili wa kijinsia ili kutokomeza tatizo hilo

Chama hicho hapa nchini kinaendesha miradi kadhaa ikiwa ni pamoja na harakati za usawa wa kijinsia na kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki vyema katika kuchangia maoni ya katiba mpya ili iwe ya demokrasia. 


WANASAYANSI UJERUMANI WAGUNDUA DAWA INAYOWEZA KUWAZUA WANAUME KUTEMBEA NJE YA NDOA

comments
FIDELITY HORMON


Wana sayansi wana mambo sikia hii huko nchini ujerumani Sasa kumegunduliwa dawa aina ya homoni inayoweza kuwazuia wanaume kwenda nje, au kuwa na uhusiano wa pembeni,

Dawa hii iliyovumbuliwa Ujerumani inaitwa FIDELITY HORMON. Dawa ya uaminifu! Au kampuni hiyo ya ujereumani imeipa dawa hiyo jina la CUDDLE DRUG! Dawa ya kukumbatiana.

Dr RenĂ© Hurle­mann, of Bonn University nchini Ujerumani anasema mwanamume akipewa dawa hii ya kumeza huyeyuka na kuingia katika damu, hivyo mwanamke mrembo akipita karibu, basi mume analazimika kukaa umbali wa inchi sita . Mume bila kujua damu yake itakuwa haipatani na mwanamke mwengine mbali na mkewe.

Mwanamke huyo akiwa mrembo zaidi , ndio dawa inafanya kazi vizuri zaidi. Ni FIDELITY HORMON. Tembe za uaminifu.Chanzo bbc


AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MISHALE NA KUKATWA MAPANGA WILAYANI TARIME AKIGOMBEA ARDHI

comments

Justus Kamugisha Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Tarime na RoryaMtu mmoja mkazi wa kijiji cha ng’ereng’ere  wilayani tarime ameuwawa kikatili kwa kuchomwa mishale na kukatwa katwa kwa mapanga .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kanda maalum ya kipolisi ya Rorya na Tarime Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha  amesema kuwa tukio hilo limetokea jana  majira ya saa mbili asubuhi  ambapo amemtaja aliyeuwawa kwa kuchomwa mishale na mapanga ni Robert  Chacha  kabila mkurya -mkira  44) mkazi  wa kijiji cha Ng’ereng’ere Kata ya Nyamaraga  Tarafa ya Inchugu wilayani Tarime.

Kamugisha amesema kuwa jeshi la polisi linamshikilia juma chacha mwita (22) wa kijiji cha  korotambe  ambaye  amekiri  kufanya hivyo na wenzake saba ambao wamekimbia na polisi wanaendelea kuwatafuta.

Chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kulima katika  eneo linalogombaniwa  na koo hizo ambapo serikali  ilikataza eneo hilo lisitumike kwa shughuli za kilimo ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara.

Kamanda  amesema kuwa baada ya Polisi kufika eneo hilo hali ya utulivu  imerejea katika vijiji vya korotambe  kubiterere ambapo kipindi cha miaka mitatu iliyopita kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara baina ya koo mbili za wanchari wakira na waryachoka  kulikuwa kunapelekea  watu kupotea maisha kuchomewa nyumba Maghala ya chakula na chanzo kikubwa ni ardhi na wizi wa Ng’ombe.
                       

SHILINGI MILIONI 800 ZATUMIKA KUNUNUA VIFAA VYA VILABU 23 VYA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

comments
Katibu Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara Beldina Nyakeke akipokea sehemu yaVifaa
Jumla ya shilingi milioni 800 zimetumika kununua vifaa vya vilabu 23 vya waandishi wa habari Tanzania bara na zanzibar vilivyoanza  kutolewa jana  na muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa lengo la kuwaongezea ufanisi wa kazi zao ambapo mikoa ya Mwanza ,Mara na Kagera imekuwa ya kwanza kukabidhiwa seti  13 ya vifaa hivyo kila mmoja.
Hafla  hiyo ya makabidhiano ya  vifaa  vya ofisi  za klabu  za waandishi wa habari  Imefanyika  jana katika ofisi za utpc jijini mwanza mtaa wa isamilo ambapo rais wa utpc keneth simbaya  alikabidhi  vifaa  vyenye thamani ya milioni  105 kwa vilabu vitatu vya mwanza,mara na kagera ambapo kila klabu thamani yake ni milioni 35  na kuwataka viongozi  waliopokea vifaa hivyo  kwenda kuvitumia kwa makini  na si kuhoziwa na viongozi  na badala yake  wapange   mipango mikakati itakayowawezesha kujitegemea kwa kubuni miradi endelevu
Awali  Rais   alisema  kuwa UTPC ilianzishwa  kwa madhumuni ya kuimarisha vilabu vya waandishi wa habari nchini ,kuchangia  kuleta maendeleo  ya  taifa sambamba na kuimarisha  demokrasia nchini  .
‘Ili mwandishi wa habari  aweze  kufanya kazi  suala la uhuru ni muhimu sana ,ukibanwa utakuwa katika kipindi kigumu ndicho tunachokipigania utpc alisema simbaya.
Alisema kuwa vifaa hivyo vinalenga kuwa endelevu  katika kazi  ambapo wanahabari watafanya kazi kwa uhuru  na kuhimili matakwa yao ya kila siku tofouti na awali kuwazimu kuazima kwa baadhi ya wadau.
‘Sisi  waandishi wa habari tunadhamana kubwa katika jamii lakini matendo yetu hayaonyeshi taswira nzuri katika jamii ,tuwe mfano  katika jamii ili tuweze  kuwa  kama mhimili wan ne wa serikali  alisema ‘’
Aidha alionya  tabia ya  baadhi ya waandishi wa habari  walioanza kugawanyika kwa kuegemea upande mmoja  badala ya kuwa pande zote kwani kazi ya  mwandishi wa habari kuielimisha jamii  ili kuleta mabadiliko ya nchi kwa kuikomboa jamii inayoteseka  vijijini  na si  kugawanyika  kunakopelekea nchi kufika  pabaya .
Vifaa vilivyokabidhiwa  ni seti 13 kwa kila  vilabu vilivyohudhuria  hafla hiyo kila  klabu imepatiwa  destop computer ,printer ,laptop computer,ups ,binding machine,lamination machine ,photocopy machine ,multimedia  projector,collapsible screen,professional still picture  camera,digital tape recorder,dvd player na tv set.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan  alisema kuwa historia kubwa imetimizwa ya ahadi ikiwa ni mojawapo ya Mkakati wa kuimarisha  vilabu ambayo tayari pia Mafunzo mbalimbali yameshatolewa na utpc nia na madhumuni ni kuwajengea uwezo wanachama wa vilabu ili kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa
Pia amewashukuru wafadhili  kutoka  sida waliowezesha kufanikisha ufadhili huo ,hivyo vilabu havina budi  kutowaangusha  kwa kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. 
Wawakiishi wa vilabu hivyo  Wakiwemo wenyeviti wa wawili  kutoka  kagera press club,mwanza press club na katibu wa mara pres club ambaye ni Mjumbe wa bodi ya UTPC  Beldina Nyakeke  wameishukuru utpc kwa msaada huo mkubwa na  wameahidi kuvilinda na kuvitunza vifaa kwani ni sehemu ya maisha yao
Kwa Hisani ya Pasco Michael na Shomari Binda

AGUNDUA ANA ALEJI NA MBEGU ZA KIUME ZA MME WAKE SIKU YA HARUSI

comments
Mike na Jullie Boyde Siku ya Harusi
Usiku wa furaha ya harusi uligeuka kuwa usiku wa majonzi baada ya wanandoa kugundua kuwa hawataweza kuwa na uwezo wa kupata mtoto katika maisha yao ya ndoa kwa kuwa bi harusi ana aleji na mbegu za kiume za mumewe.Mike mwenye umri wa miaka 27 na Julie Boyde mwenye umri wa miaka 26 wakazi wa Ambridge, Pennsylvania nchini Marekani walikuwa katika mapenzi moto moto kwa miaka miwili kabla ya kuamua kufunga ndoa na kuamua kufanya mapenzi bila kutumia kinga kwa mara ya kwanza usiku wa harusi yao.

Lakini mambo hayakuenda vizuri kama walivyotarajia kwani ghafla iligundulika kuwa bi harusi alikuwa na aleji na mbegu za kiume za mumewe.

Muda mfupi baada ya Mike kuziachia mbegu zake za kiume, Bi harusi alipatwa na maumivu makali sana ambayo mwenyewe anayaelezea kuwa ni sawa na kama mtu alikuwa akipigilia misumari ndani ya mwili wake.

Maumivu hayo yaliyoambatana na vipele yaliendelea kwa wiki kadhaa kabla ya kutoweka.

Baada ya vipimo kadhaa vya madaktari iligundulika kuwa Julie ana aleji na mbegu za kiume za Mike.

Madaktari walisema kwamba mwili wa Julie huzichukulia mbegu za kiume za Mike kama protini ambazo hazikubaliki kwenye mwili wake na hivyo kuufanya mwili wake kuzishambulia mbegu hizo za kiume.

Hali aliyo nayo Julie imewafanya wanandoa hao wapya waghairi mpango wao wa kupata mtoto kwasababu uwezekano wa Julie kushika ujauzito ni finyu kwa kuwa mwili wake huzishambulia na kuziua mbegu za kiume kila zinapoingia kwenye mwili wake.

Mike na Julie walianza mapenzi yao wakati wakiwa chuo kikuu na walivalishana pete za uchumba miaka miwili baadae na mwishoe mwaka 2005 waliamua kufunga ndoa.

Lakini baada ya sherehe za kuisha na walipotaka kulila tunda kwa mara ya kwanza bila ya kutumia kondomu wakiwa kama mke na mume , usiku wa harusi ulibadilika ghafla na kuwa usiku wa majonzi.

"Kabla ya kuoana tulikuwa makini na tulitumia kondomu wakati wote, siku ya harusi hatukutaka kutumia kondomu", alisema Julie.

"Kwakuwa tulikuwa tumeishafunga ndoa hatukuona sababu ya kuogopa kupata ujauzito".

"Na ndipo nilipopatwa na maumivu makali sana kama vile mtu ananichoma moto muda mfupi baada ya Mike kuniachia mbegu zake za kiume", aliendelea kusema Julie.

"Hali ilikuwa inatisha sana, maumivu yaliendelea kunisumbua kwa wiki kadhaa".

Baada ya njia mbali mbali za kutibu tatizo hilo, zote kufeli, wanandoa hao wapya kwa kujua kuwa hawana uwezo wa kupata mtoto, wameanza taratibu za kutafuta mtoto watakayejitolea kumlea kama mtoto wao.

Mkasa wa maisha yao umetengenezewa documentary na televisheni ya Discovery Channel na documentary hiyo iliyopewa jina la "Strange Sex" itarushwa hewani nchini Marekani. Chanzo Nifahamishe
 

 

MUSOMA YAPATA MABILIONI TOKA BENKI YA DUNIA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO MUSOMA MJINI

comments

HALMASHAURI ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara, imepata msaada wa zaidi ya sh bilioni 21 kutoka Benki ya Dunia (WB).

Fedha hizo zitaanza kutolewa Julai mwaka 2013 na zitatolewa kwa miaka mitatu ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Musoma mjini.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Kisurura, alisema hayo jana mjini hapa alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu mipango ya maendeleo kwa wakazi wa mji huo na kujinasibu kwamba katika kipindi cha miaka mitano manispaa hiyo itafurahia mafanikio ya kisekta.

Kwa mujibu wa mstahiki huyo fedha hizo za ufadhili wa Benki ya Dunia zimelenga kutekeleza miradi ya kiuchumi ikiwemo miundombinu ambapo kila mwaka benki hiyo itatenga fedha ili kufikia malengo ya maendeleo.

“Manispaa ya Musoma tumekubaliwa na Benki ya Dunia kupewa dola milioni 14.1 za Marekani kuanzia Julai 2013 na tutapewa kwa awamu tatu kila mwaka wa fedha!

“…Licha ya Benki ya Dunia kutupa fedha hizi imetupa masharti ya kuhakikisha matumizi yake yanakuwa ya wazi, ukusanyaji wa mapato uwe mzuri. Ufadhili huu utaishia mwaka 2018; naamini muda huo Musoma itakuwa mbali kimaendeleo,” alisema meya huyo.

Hata hivyo, alizitaja halmashauri za Geita, Bariadi, Manispaa ya Bukoba na Shinyanga kuwa ni miongoni mwa halmashauri zilizoomba na kupewa ufadhili wa aina hiyo lakini manispaa yake imepata fedha nyingi zaidi kwa ukanda wa Ziwa Victoria.
Chanzo: Tanzania Daima

ALIYE KUWA WAZIRI WA KWANZA WA SHERIA NCHINI UFARANSA RACHIDA DATI ADAI KUWA HAJUI NANI BABA WA MTOTO WAKE KWA KUWA ALIKUA NA MAHUSUANO YA KIMAPENZI NA WANAUME WANANE KWA KIPINDI KIMOJA

comments
Rachida Dati
Aliyekuwa waziri wa kwanza mwanamke wa sheria nchini Ufaransa, Rachida Dati amedaiwa kuwa hajui nani ndiye baba wa mtoto wake kwakuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na wanaume wanane kwa kipindi kimoja.


Rashida Dati mwenye umri wa miaka 47 amedaiwa kuwa alikuwa bize kwenye kubadilisha mabwana kiasi cha kwamba hajui ni mwanaume gani ndiye aliyempa mimba.

Dati amemfikisha mahakamani bilionea Dominique Desseigne, 68, akidai ndiye baba wa binti yake Zohra kufuatia uhusiano wao wa kimapenzi mnamo mwaka 2008.

Desseigne amegoma kupima DNA akisema kuwa yeye alikuwa miongoni mwa wanaume wanane waliokuwa wakitembea na waziri huyo wa zamani wa sheria nchini Ufaransa.

Katika ushahidi wa maandishi uliotolewa na wanasheria wa bilionea Desseigne umeweka wazi kuwa Dati alikuwa na mahusiano na wanaume wanane katika kipindi kimoja na imewataja wanaume hao kuwa miongoni mwao yumo aliyekuwa waziri mkuu wa Hispania, Jose Maria Anzar na aliyekuwa rais wa Ufaransa, Sarkozy.

Pia katika listi hiyo yumo kaka wa rais huyo wa Ufaransa na pia yumo mwanasheria mkuu wa Qatari na matajiri wengine maarufu.

Sheria za Ufaransa zinamruhusu mtu kugoma kupima DNA kwenye kesi kama hizi za madai ya watoto.

Dati alichaguliwa kuwa waziri wa sheria mnamo mwaka 2007 lakini alifukuzwa kazi mwaka 2009 baada ya kuonekana utendaji wake wa kazi ni mbovu.Chanzo Nifahamishe

MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MARA YAVUKA LENGO KATIKA UKUSANYAJI KODI TOKA MWEZI JULAI HADI OCTOBA 2012

comments
TANZANIA REVENUE AUTHORIRTY              


Mamlaka ya Mapato ya Mkoa wa Mara imevuka  malengo  kwa kukusanya  kiasi cha shilingi bilioni 23. na kuvuka  lengo lililokusudiwa  la shilingi bilioni 22.2 kwa kipindi cha julai hadi oktoba 2012.

Hayo yamesemwa  leo na meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mara Joseph Kalinga  wakati akitoa taarifa  ya ukusanyaji wa mapato  kwa mgeni rasmi katibu tawala wa Mkoa wa Mara Clement Lujaji .

Kalinga amesema kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma  yenye  ubora wa hali ya juu na  ya kuvutia  kwa mlipakodi  , idara ya huduma  na elimu  kwa mlipa kodi ,imekuwa  ikitoa semina mbalimbali zenye lengo la kuwaelimisha  walipa kodi sheria  za kodi ,haki za mlipa kodi,wajibu wa mlipa kodi na wajibu wa mamlaka ya mapato imeongeza ushirikiano  baina ya walipa kodi  na watoza  kodi  pamoja  na kuinua  kiwango cha ulipaji  kodi kwa hiari.

Amesema kuwa hali ya makusanyo  kwa mwaka wa fedha wa 2011/12,Mkoa wa Mara ni sawa na asilimia 86 ya lengo lililowekwa hapo awali la kukusanya shilingi bilioni 63.5 kwa kuwa mamlaka imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 54.7

Aidha  kalinga ameelezea changamoto zinazowakabili ni pamoja ongezeko la mahitaji ya mapato  ya serikali katika kutekeleza  mikakati  yake  ya kupambana na umasikini ,ukwepaji kodi kwa kupitia  njia zisizo  rasmi  wakati wa kuingiza  bidhaa nchini  au kutoa bidhaa kwenda nje ya nchi,ukwepaji kodi  kwa njia ya kutotoa risti sambamba na matumizi hafifu ya mashine  za kutolea  risti  EFD) kwa wasiosajiliwa katika kodi ya ongezeko  la thamani  VAT.

Mamlaka kwa kushirikiana  na vyombo vingine  vya uthibiti  ambavyo ni jeshi la polisi ,usalama wa taifa na uhamiaji  vimeweka  mkakati  wa kukabiliana na changamoto  inayohusu  ukwepaji kodi  kwa kutumia njia mbalimbali.

Kwa upande wake mgeni rasmi  katibu tawala wa mkoa wa Mara Clement Lujaji  amesema kuwa dhana ya ulipaji kodi kwa hiari inalenga uelewa wa mlipaji kodi yeye mwenywe na maendeleo ya taifa na jamii nzima ambapo amesema kuwa  kukwepa kodi ni aibu  na sio ujasiri ,hivyo amewataka mamlaka ya mapato kupanua eneo la hamasa kuanzia ngazi ya kata  kwa kuwashirikisha madiwani ili kuongeza walipa kodi, kauli mbiu ulipaji kodi kwa hiari kwa mafanikio ya taifa.

''walipa kodi ni sisi tukilipa  kodi tutaona  zahanati zinajengwa ,shule tra panueni wigo  kutolipa kodi ni aibu'' alisema lujaji.

TIMU YA WAANDISHI WA HABARI YAITANDIKA TRA MARA 2-1 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI KUELEKEA KUADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI

comments

Benchi la ufundi likifuatilia kwa umakini kambumbu kutoka kushoto ni Emmanuel Almas, George Marato, Shomari Binda,Thomas Dominick na Emmanuel Chibasa

Wachezaji wa Timu ya waandishi wa habari wakisherekea ushindi mara baada ya mpira kumalizika kati yao kuanzia Kulia ni Denis Magoti,dj Cares One,Dj Lima wakionyesha ishara ya bao 2 na anaefuata ni Opudo ambaye anaonyesha ishara ya Tano kwa timu tutakayo cheza nayo tenana mwisho ni Golikipa mahiri

 

Kikosi cha Timu ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mara Kabla ya mechi

Timu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara Ambayo ilianza kipindi cha Kwanza Katika uwanja wa Posta Musoma Ambapo Timu hiyo iliibuka na ushindi 2-1

Timu ya waandishi wa habari mkoani mara jana imeibuka na mshindi katika mchezo dhidi ya Timu ya mamlaka ya mapato Tanzania mkoani hapa kwa jumla ya mambo 2-1 katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Posta manspaa ya musoma.

Timu ya Mamlaka ya mapato ndio walikua wa kwanza kuliona lango la Waandishi wa habari katika kipindi cha kwanza katika mchezo huo ambao ulikua na upinzani mkubwa.

Katika kipindi cha pili timu ya waandishi wa habari ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wako hali iliyozaa mamtunda baada ya timu hiyo kufanikiwa kupata bao kwa njia ya penati kupitia kwa mchezaji wake Paul Peter baada ya mchezaji kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika timu ya waandishi wa habari ilifanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa Alhaj Majogoro na kupelekea mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu ya waandishi wa habari 2 na timu ya mamlaka ya mapato mkoa wa mara 1.

Timu ya waandhi wa habari imekabidhiwa kombe leo katika kilele cha siku ya mlipa kodi sherehe ambazo zimefanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkendo.

AMSHITAKI MKEWE BAADA YA KUZAA MTOTO MWENYE SURA MBAYA, ASHINDA KESI ALIPWA MAMILIONI YA PESA

comments
Hii ndo Picha ya Mwanamke huyo anaonekana kabla na baada ya kufanyiwa Oparesheni

Mwanaume mmoja nchini China alishtuka baada ya mkewe kuzaa mtoto mwenye sura mbaya na aliamua kumfikisha mkewe mahakamani kwa kutomjulisha kuwa sura yake nzuri ilitokana na operesheni za kubadilisha sura, alishinda kesi na kuzawadia fidia ya mamilioni.


Wakati Jian Feng alipomuona mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza alishtuka sana.

Mtoto wake huyo wa kike alikuwa na sura mbaya kiasi cha kwamba alishindwa kuamini kuwa mkewe aliyekuwa akionekana mrembo sana angeweza kuzaa mtoto kama huyo.

Jian alimgeuzia kibao mkewe na kumshtumu kuwa aliisaliti ndoa yao na kufanya mapenzi nje ya ndoa yaliyopelekea kuzaliwa kwa mtoto huyo.

Baada ya hali kuwa tata, mkewe alilazimika kutoboa siri kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni zilizomgharimu zaidi ya dola 100,000 ili kuirekebisha sura yake aonekane mrembo. Mkewe alisisitiza kuwa mtoto huyo ni wa kwao.

Jian alikasirika sana kusikia hivyo na kuamua kumfikisha mkewe mahakamani akidai kuwa alirubuniwa kuingia kwenye ndoa na alidai fidia ya mamilioni ya pesa.

"Nilimuoa mke wangu kwa mapenzi makubwa kwa jinsi alivyokuwa akionekana lakini punde baada ya kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza matatizo yalianza kwenye ndoa yetu", alisema Jian.

"Binti yetu alikuwa na sura mbaya sana kiasi cha kwamba nilitishika sana", Jian aliwaambia wanasheria wake kuwa mkewe alimvuta kwenye ndoa kwa kufanya operesheni ya kutengeneza sura yake aonekane mrembo na kuzaliwa kwa mtoto wao huyo ndiko kulikopelekea ukweli kujulikana.

Mahakama ilikubaliana na madai ya Jian na kuamua alipwe fidia ya dola 120,000 ( zaidi ya Tsh. milioni 170) baada ya mkewe kukiri kuwa hakuwahi kumwambia mumewe kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni.

Mahakama ilimuona mkewe ana hatia ya kumrubuni Jian kuingia kwenye ndoa na ilikubali maombi ya Jian ya kuivunja ndoa hiyo.Chanzo:Nifahamishe
  

JOHN MNYIKA ATOA WITO KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUTOA RASIMU YA SERA YA GESI ASILIA KWA LUGHA YA KIINGEREZA NA KISWAHILI

comments
Mbuge wa Ubungo John Mnyika
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), amepingana na hatua ya Wizara ya Nishati na Madini kutoa rasimu ya sera ya gesi asilia kwa Lugha ya Kiingereza pekee na kutoa wito sera hiyo kuandikwa pia katika lugha ya Kiswahili.

Mnyika alisema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana na kumtaka Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo, kuutangazia umma kwamba, rasimu hiyo itatolewa pia kwa lugha ya Kiswahili na kwamba, ichapwe katika vyombo vingine vya habari.

“Izingatiwe kuwa napinga hatua ya Wizara ya Nishati na Madini kuchapa rasimu ya Sera ya Taifa ya Gesi Asili kwa Lugha ya Kiingereza pekee kwenye baadhi ya magazeti tarehe 2 Novemba 2012, huku Katibu Mkuu wa Wizara hiyo akitoa mwito kwa wadau na Watanzania wote kutoa maoni hali, ambayo itakuwa ni kikwazo kwao kushiriki katika mchakato wa maandalizi ya sera yenye kuzingatia maslahi ya taifa,” alisema Mnyika katika taarifa hiyo.

Alisema kitendo cha Bodi mpya ya Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kusogeza mbele muda wa kukamilisha ripoti yao kutoka Septemba 30 hadi Novemba 30, mwaka huu, kutakosesha nafasi ya kutoa maoni ya kuboresha rasimu hiyo ya sera kwa madai kwamba, matokeo ya mapitio hayo yanafanyika kwa kutumia fedha za umma.

Alimtaka Waziri Muhongo kutumia fursa hiyo kuweka hadharani matokeo ya agizo lake la kupitiwa upya kwa mikataba yote 26 ya utafutaji mafuta na gesi asili ili udhaifu uliobainika kwenye mikataba hiyo utumiwe na umma kutoa maoni na mapendekezo ya kuboresha sera, sheria, taasisi na mfumo mzima wa uingiaji wa mikataba.

Mnyika, ambaye pia ni Waziri Kivuli katika Wizara ya Nishati na Madini, alimtaka Waziri Muhongo kueleza namna kamati mbalimbali za kudumu za Bunge zitakavyohusishwa katika mchakato wa kukusanya maoni pamoja na kuishauri na kuisimamia serikali kutokana na unyeti wa sera hiyo.

Chanzo:ipp media

MWANACHUO WA CHUO CHA MUSOMA UTALII ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA KUMCHOMA VISU MWANACHUO MWENZAKE KISA WIVU WA KIMAPENZI

comments
Mwanachuo wa chuo cha musoma utalii cha mjini Musoma Rose Kanyambo (21),ameshambuliwa kwa kisu mgongoni na ubavuni na mwanachuo mwenzake John Ogolla kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Taarifa toka kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mara Irege Ngaregeza, amesema kuwa binti huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya ijumaa Novemba 2 mwaka huu, ambapo binti huyo alikuwa na jeraha la kuchomwa kisu mgongoni na ubavuni na alifikishwa hospitalini hapo akiwa na hali mbaya lakini madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake na sasa anaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa taabu wodini binti huyo amesema kuwa siku ya ijumaa majira ya saa mbili asubuhi akiwa chuoni maeneo ya Kamunyonge manispaa ya musomaMwanachuo mwenzake anaefahamika kwa jina John Ogolla alitokea  chuoni hapo na kuanza kumshambulia kwa kumchoma kisu mgongoni mara mbili  na ubavuni ambpo hali hiyo ilimpelekea kutokwa na damu nyingi ambapo alifanikiwa kukimbia hadi alipokuwa anaishi si mbali na chuo lakini kabla hajafika nyumbani alidondoka chini baada ya kuishiwa nguvu  lakini majirani walifanya jitihada za kumpeleka hospitalini.

Binti huyo amewambia waandishi wa habari kuwa chanzo cha tukio hilo la kinyama la kuchomwa kisu ni kumkataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo na mara kwa mara amekuwa akimlazimisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini yeye amekuwa akimkatalia.

Baadhi ya majirani na wanachuo ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamesema kuwa  Rose na John wanauhusiano wa kimapenzi kwa  muda mrefu na kijana huyo amekuwa akimsaidia  mambo mengi sana lakini ghafla mpenzi huyo alibadilika na kumkataa bila sababu za msingi hali iliyopelekea kijana huyo kuchukua maamuzi hayo mazito ya kumchoma kisu.

"kabla yaOgolla kutekeleza tukio hilo alikuwa ameandaa barua ambayo ameandika yenye ujumbe uliosomeka ama kufa yeye au rose kanyambo na pia alichukua picha ambayo walipiga pamoja na Rose na kuichora alama ya x kwa kutumia marker pen" alisema shuhuda

Jeshi la polisi linamshikilia john ogolla kuhusiana na tukio na mara baada ya upelelezi kukamilika atapandishwa kizimbani.

MREMBO KUTOKA MARA ASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA FAINALI ZA REDDS MISS TANZANIA 2012 HONGERA HOMELAND ENTERTAINMENTS

comments
Shindano la kumtafuta Mrembo wa Redds Miss Tanzania 2012 limemalizika siku ya Jumamosi huku mrembo Brigette Alfred kutoka Kitongoji cha Sinza, ameibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Pearl Pub, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Mrembo huyo kutoka kituo cha Sinza na baadaye kuingia katika shindano la Kanda ya Kinondoni, kwa ushindi huo amejitwalia zawadi ya gari aina ya Noah na kitita cha sh milioni 8 zilizotolewa na mdhamini mkuu wa shindano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

Mshindi wa pili katika shindano hiloni Eugine Fabian kutoka Mara alijipatia sh milioni 6.2 akifuatiwa na Edda Sylvester kutoka Kitongoji cha Kigamboni, Kanda ya Temeke, aliyeondoka na sh milioni 4.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Magdalena Roy aliyeondoka na sh milioni 3 na Happiness Daniel alishika nafasi ya tano na kujitwalia sh milioni 2.4.

Walishika nafasi ya sita hadi 15, kila mmoja alijinyakulia sh milioni 1.2 na washiriki wengine waliobaki kila mmoja atajipoza kwa sh 700,000.

Kwa ushindi huo, Brigitte ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia, yatakayofanyika mapema mwakani, huku akitegemewa kufanya makubwa zaidi kutokana na maandalizi ya muda mrefu atakayopewa.
Kwa mara ya kwanza katika shindano hilo mwaka huu, warembo watano kati ya 30 waliingia moja kwa moja hatua ya 15 bora, baada ya kutwaa mataji tofauti yaliyokuwa yakiwaniwa na warembo wote 30 kabla ya fainali.

Warembo wengine waliotinga 15 bora ni Babylove Kalala, Mary Frank, Happiness Rweyemamu, Joyce Baluhi, Edda Sylvester, Brigette Fina Revocatus, Catherine Masumbigana, Irene Veda na Eugene Fabian.
Wengine ni Lucy Stephano aliyeshinda Miss Photogenic, Mary Chizi (Miss Sports Lady), Babylove Kalala (Miss Talent), Magdalena Roy (Top Model) na Happiness Daniel aliyetwaa taji la Miss Personality.
Shindano hilo, lilipambwa vilivyo na wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond’, Winfrida Josephat ‘Recho’ na kundi la Wanne Star.

KUACHWA KUACHWA KUACHWA NI SHUGULI PEVU

comments
Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ambaye hakuridhishwa na uamuzi wa mpenzi wake kuachana naye, aliamua kumaliza hasira zake kwa kuzamisha meno yake kwenye uume wa mpenzi baada ya kujifanya anaomba msamaha ili uhusiano wao uendelee.


Sinead Walker, mwenye umri wa miaka 40 mkazi wa Bath, Somerset nchini Uingereza alienda kwa mpenzi wake kwaajili ya kuomba msamaha ili mapenzi yao yaendelee kama zamani.

Lakini ghafla mwanamama huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja, alibadili uamuzi wake wa kuomba msamaha na kuamua kumshambulia mpenzi wake Vincent Rennoldson mwenye umri wa miaka 42 kwa kuyabinya kwa nguvu makende yake kabla ya kuamua kuzamisha meno yake ili aukate uume wake.

Mahakama ambayo inasikiliza kesi ya mama huyo kujaribu kuzinyofoa hazina za mpenzi wake, iliambiwa kuwa Sinead akiwa amelewa alienda nyumbani kwa mpenzi wake akisema amekuja kuomba msamaha baada ya kumshambulia Vincent wiki mbili zilizopita baada ya Vincent kuamua kuvunja uhusiano wao.

"Alinisukuma ukutani, aliukamata uume wangu na kuanza kuuvuta kwa nguvu akijaribu kuunyofoa baadae alizamisha meno yake kwenye uume wangu na kuniachia kovu kubwa", alisema Vincent.

Vincent aliongeza kuwa Sinead alikuwa amepiga magoti akijifanya kuomba msamaha kabla ya kuanza shambulio lake hilo.

"Maumivu yake hayaelezeki, nilitokwa na damu nyingi sana, angeweza kuunyofoa kabisa uume wangu", Vincent aliiambia mahakama.

Vincent alielezea kusikitishwa kwake na kitendo hicho ingawa alidai anashukuru mambo hayajaharibika sana na uume wake unafanya kazi kama kawaida.

Sinead atahukumiwa mwezi ujao, ameachiwa kwa dhamana huku akitakiwa asimkaribie mpenzi wake huyo wa zamani

chanzo:Nifahamishe

SIMU BANDIA UGANDA KUZIMWA 2013 TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI PIA WAJADILI KUKAMILISHA ZOEZI HILO

comments: 1
Uganda inachukua hatua Sawa na Kenya ambayo ilizima simu za watu zaidi ya Milioni Moja
Uganda imeamua kusitisha mipango yake ya kuzima simu ghushi hadi tarehe moja mwezi Julai mwaka 2013.
Hatua ya serikali inayolenga kuzuia simu bandia kutumika katika mitandao ya simu nchini humo ilikuwa imepangiwa kuafikiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Tume ya mawasiliano ya Uganda, imependekeza kuwa takriban asilimia kumi na tatu ya simu milioni kumi na saba za rununu Afrika Mashariki ni ghushi.

Watumiaji wa simu hizo, wana hadi mwezi Machi kuhakikisha kuwa kadi zao zimesajiliwa na tume hiyo.
Pia wametakiwa kubaini nambari yao ya kutambua simu ijulikanayo kama IMEI (International Mobile Equipment Identity) na ambayo huwa ipo kwenye simu halali. Simu ghushi kawaida huwa hazina nambari hii ya utambulisho.

Tume hiyo ya mawasiliano inasema kuwa hatua ya serikali itasaidia maafisa wa sheria kuwasaka wahalifu wanaotumia simu bandia.
Rwanda, Burundi na Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yamejadili mipango ya kuzima simu ghushi.

Simu bandia ni maarufu kwa sababu zina bei nafuu kuliko simu halali mara nyingi kwa sababu wanaoziuza huwa wamekwepa kulipa kodi.

Lakini maafisa wanasema kuwa zinaweza kusababisha athari kubwa za kiafya. Wanasema simu hizo hazijafanyiwa utafiti ikiwa ni salama .

Pia wameongeza kuwa simu hizo hazijatengezwa katika njia ambayo inaweza kutumika kwa mitandao ya simu,kwani zinaweza kusababisha simu kukatika mara kwa mara.
chanzo:bbc swahili
comments
Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Asalom Mwakyoma
Mtu  mmoja  asiyefahamika majina amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwa na panga  katika kijiji cha magunga kata ya buhemba wilayani butiama mkoani mara

Kamanda wa polisi wa mkoa wa mara ,kamishina msaidizi Absalom Mwakyoma amethibitisha tukio hilo ambapo jeshi hilo linafanya uchunguzi ili kubaini marehemu huyo kuwa ni mkazi wa wapi,ambapo mwili wake umeletwa kuhifadhiwa katika chumba cha maiti musoma.

Wakati huo usiku wa kuamkia leo watu wasiofahamika  wamevamia nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo kwa jina la yote heri iliyoko buhemba wakiwa na silaha aina ya smg huku wakijitambulisha kuwa ni askari polisi  na kuwaamuru wateja wote kufungua milango na kuwapora  simu na fedha na baada ya kutekeleza wizi huo watu hao walitokomea kusikojulikana.

Jeshi la polisi mkoani mara linaendelea kuwasaka majambazi hayo ambapo pia limewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kuwasaka watuhumiwa.
  
Huko wilayani bunda askari wa jeshi la polisi na familia zao wilayani Bunda mkoani Mara wameingia katika adha kubwa ya kulazimika kutumia  tochi, vibatari na mishumaa kwa kukosa umeme takriban mwezi mmoja sasa.

Hatua hiyo imekuja kutokana na taasisi hiyo kushindwa kununua luku za umeme kwa matumizi ya ofisi  na katika makazi ya askari hao.

Kwa sharti ya kutotajwa majina baadhi ya askari hao jana wamewaeleza waandishi wa habari waliofika kituoni kujionea hali kuwa umeme unaotumika katika kituo hicho  hulipwa na baadhi ya viongozi wa kituo kwa kujitolea.

Walisema katika makazi yao hali ni mbaya zaidi kutokana na serikali kutowapelekea fedha za kununua umeme.

“ tunaishi maisha ya shida sana maana kama kambi ya polisi wanaolinda usalama wa raia tunakosa umeme ni hatari  hata kwa usalama wetu” alisema askari mmoja.

Meneja wa Tanesco wilaya ya Bunda Sosthenes  Lushamisa alidai kuwa  tatizo la polisi kutokuwa na umeme ni lao wenyewe kutokana na kutonunua LUKU katika  mita ya TANESCO waliyofungiwa katika kambi yao.

Bw. Lushamisa alifafanua kuwa askari hao wana matumizi makubwa ya umeme lakini wanashindwa kununua umeme wa kutosha na kwa wakati.

Alidai Shirika lake halina tatizo labda la kiufundi jambo ambalo bado hawajapata malalamiko yoyote kutoka polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalum Mwakyoma alipoulizwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi alidai kuwa hana taarifa zozote za polisi Bunda kukosa umeme huku akiahidi kufuatilia.

Wananchi wanaoishi karibu na kambi hiyo wamesikitishwa na kambi la polisi kukaa gizani jambo ambalo ni hatari kwa ulinzi na usalama na kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo.