AGUNDUA ANA ALEJI NA MBEGU ZA KIUME ZA MME WAKE SIKU YA HARUSI

Mike na Jullie Boyde Siku ya Harusi
Usiku wa furaha ya harusi uligeuka kuwa usiku wa majonzi baada ya wanandoa kugundua kuwa hawataweza kuwa na uwezo wa kupata mtoto katika maisha yao ya ndoa kwa kuwa bi harusi ana aleji na mbegu za kiume za mumewe.



Mike mwenye umri wa miaka 27 na Julie Boyde mwenye umri wa miaka 26 wakazi wa Ambridge, Pennsylvania nchini Marekani walikuwa katika mapenzi moto moto kwa miaka miwili kabla ya kuamua kufunga ndoa na kuamua kufanya mapenzi bila kutumia kinga kwa mara ya kwanza usiku wa harusi yao.

Lakini mambo hayakuenda vizuri kama walivyotarajia kwani ghafla iligundulika kuwa bi harusi alikuwa na aleji na mbegu za kiume za mumewe.

Muda mfupi baada ya Mike kuziachia mbegu zake za kiume, Bi harusi alipatwa na maumivu makali sana ambayo mwenyewe anayaelezea kuwa ni sawa na kama mtu alikuwa akipigilia misumari ndani ya mwili wake.

Maumivu hayo yaliyoambatana na vipele yaliendelea kwa wiki kadhaa kabla ya kutoweka.

Baada ya vipimo kadhaa vya madaktari iligundulika kuwa Julie ana aleji na mbegu za kiume za Mike.

Madaktari walisema kwamba mwili wa Julie huzichukulia mbegu za kiume za Mike kama protini ambazo hazikubaliki kwenye mwili wake na hivyo kuufanya mwili wake kuzishambulia mbegu hizo za kiume.

Hali aliyo nayo Julie imewafanya wanandoa hao wapya waghairi mpango wao wa kupata mtoto kwasababu uwezekano wa Julie kushika ujauzito ni finyu kwa kuwa mwili wake huzishambulia na kuziua mbegu za kiume kila zinapoingia kwenye mwili wake.

Mike na Julie walianza mapenzi yao wakati wakiwa chuo kikuu na walivalishana pete za uchumba miaka miwili baadae na mwishoe mwaka 2005 waliamua kufunga ndoa.

Lakini baada ya sherehe za kuisha na walipotaka kulila tunda kwa mara ya kwanza bila ya kutumia kondomu wakiwa kama mke na mume , usiku wa harusi ulibadilika ghafla na kuwa usiku wa majonzi.

"Kabla ya kuoana tulikuwa makini na tulitumia kondomu wakati wote, siku ya harusi hatukutaka kutumia kondomu", alisema Julie.

"Kwakuwa tulikuwa tumeishafunga ndoa hatukuona sababu ya kuogopa kupata ujauzito".

"Na ndipo nilipopatwa na maumivu makali sana kama vile mtu ananichoma moto muda mfupi baada ya Mike kuniachia mbegu zake za kiume", aliendelea kusema Julie.

"Hali ilikuwa inatisha sana, maumivu yaliendelea kunisumbua kwa wiki kadhaa".

Baada ya njia mbali mbali za kutibu tatizo hilo, zote kufeli, wanandoa hao wapya kwa kujua kuwa hawana uwezo wa kupata mtoto, wameanza taratibu za kutafuta mtoto watakayejitolea kumlea kama mtoto wao.

Mkasa wa maisha yao umetengenezewa documentary na televisheni ya Discovery Channel na documentary hiyo iliyopewa jina la "Strange Sex" itarushwa hewani nchini Marekani. Chanzo Nifahamishe
 

 

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE