commentsEmmanuel Chibasa-Mara

Watu wenye ulemavu mkoani Mara wamekutana na uongozi wa mkoa wakiwemo madiwani, wakuu wa idara, pamoja na maafisa maendeleo ya jamii, lengo ikiwa ni kuitambulisha  miongozo ya kitaifa na kimataifa inayoelezea mahitaji na hali halisi ya watu wenye ulemavu ili waweze waweze kuingizwa kwenye mipango kazi pamoja na Bajeti za Halmashauri.

Akiongea katika kikao hicho Abdala Omari ambaye ni mmoja ya wajumbe ya wajumbe wa chama cha walemavu Tanzania SHIVYAWATA ,amesema wameamua kutambulisha miongozo hiyo ili kupunguza changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kwa kuingizwa kwenye bajeti za Halmashauri hapa nchini ili kuondokana na utegemezi katika jamii.

INSERT: Abdala Omary-Mjumbe Shivyawata

Batista Mgumba ni mwezeshaji kutoka chama cha wasioona Tanzania amesema imefika wakati maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania inatakiwa yaingizwe kwenye bajeti za halmashauri wakati wa kupanga mipango pamoja na kupanga bajeti ili waweze kupata huduma sawa kama walivyo watu wengine.

INSERT: Batista Mgumba-Mwezeshaji Chama cha Wasioona Tanzania

Kwa upande wake mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu Elieza Mdakilwa amesema kutokana na watu kutokua na mwamko wa kutetea haki za watu wenye ulemavu hapa mchini ametoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na maswala ya watu wenye ulemavu zinatakiwa kuendelea kutetea haki za watu wenye ulemavu kunzia ngazi ya serikali za mitaaa mpaka serikali kuu.

INSERT: Elieza Mdakilwa-Mwanaharakati

Takwimu zinaonyesha kuwa  mkoa wa Mara unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu hapa nchini kwa kuwa  asilimia 13.
Mwisho

comments


25 Oct 2014

TIMU ya Polisi Mara imeondoka kuelekea mkoani Shinyanga kucheza mchezo wake wanne dhidi ya timu ya Mwadui huku ikitoa tambo ya kufanya mizuri kwenye mchezo huo kutokana na uelewano wa wachezaji.

Akizungumza kabla ya kuondoka kwa timu hiyo yenye maskani yake mjini musoma Afisa Habari wa timu hiyo Musa Keita amesema timu hiyo inaenda kucheza mchezo wa ugenini ikiwa na pointi 7 ikiwa ni ushindi wa michezo miwili na sare moja katika michezo iliyotangulia imewaweka wachezaji katika ari nzuri ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Amesema kwa sasa kikosi cha timu hiyo kipo kwenye maelewano mazuri uwanjani ndio sababu inayowapa Imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa dhidi ya Mwadui hapo kesho.

Keita alisema wanaondoka kwenda kwenye michezo ya ugenini wakiamini kufanya vizuri kuanzia mchezo huo dhidi ya Mwadui kabla ya kuzifuata timu za JKT Kanembwa na polisi ya Tabora na baadae kurudi nyumbani kwenye michezo mingine.

Akizungumzia michezo mitatu iliyotangulia na kujipatia pointi 7,alisema licha ya timu kufanya vizuri lakini pia wanawashukuru wadau wa soka mkoani Mara kuwapa sapoti kwa kila mchezo na kuomba ushirikiano huo uendelee ili timu hiyo iweze kufanya vizuri kwenye michezo mingine.

Katika michezo iliyotangulia Timu ya polisi Mara ilianza kugawana pointi na timu ya Rhino ya Tabora kwa kufungana bao 1-1 kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya timu ya Green Worrers ya Dar es salaam na Burkinafaso ya Morogoro.