Emmanuel
Chibasa-Mara
Watu wenye
ulemavu mkoani Mara wamekutana na uongozi wa mkoa wakiwemo madiwani, wakuu wa
idara, pamoja na maafisa maendeleo ya jamii, lengo ikiwa ni kuitambulisha miongozo ya kitaifa na kimataifa inayoelezea
mahitaji na hali halisi ya watu wenye ulemavu ili waweze waweze kuingizwa
kwenye mipango kazi pamoja na Bajeti za Halmashauri.
Akiongea
katika kikao hicho Abdala Omari ambaye ni mmoja ya wajumbe ya wajumbe wa chama
cha walemavu Tanzania SHIVYAWATA ,amesema wameamua kutambulisha miongozo hiyo
ili kupunguza changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu kwa kuingizwa kwenye
bajeti za Halmashauri hapa nchini ili kuondokana na utegemezi katika jamii.
INSERT: Abdala Omary-Mjumbe
Shivyawata
Batista
Mgumba ni mwezeshaji kutoka chama cha wasioona Tanzania amesema imefika wakati
maswala ya watu wenye ulemavu Tanzania inatakiwa yaingizwe kwenye bajeti za
halmashauri wakati wa kupanga mipango pamoja na kupanga bajeti ili waweze
kupata huduma sawa kama walivyo watu wengine.
INSERT: Batista Mgumba-Mwezeshaji
Chama cha Wasioona Tanzania
Kwa upande
wake mwanaharakati wa kutetea haki za watu wenye ulemavu Elieza Mdakilwa
amesema kutokana na watu kutokua na mwamko wa kutetea haki za watu wenye
ulemavu hapa mchini ametoa wito kwa taasisi zinazojihusisha na maswala ya watu
wenye ulemavu zinatakiwa kuendelea kutetea haki za watu wenye ulemavu kunzia
ngazi ya serikali za mitaaa mpaka serikali kuu.
INSERT: Elieza Mdakilwa-Mwanaharakati
Takwimu
zinaonyesha kuwa mkoa wa Mara unaongoza
kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wenye ulemavu hapa nchini kwa kuwa asilimia 13.
Mwisho
Comments
Post a Comment