KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

Kati ya Kuku na Yai Kipi Kilianza?

Mjadala wa miaka mingi kuhusiana na kipi kilitokea mwanzo kuku au yai? umepata jibu baada ya wanasayansi kuthibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo awali kabla ya yai.



Mjadala wa miaka nenda rudi kuwa kuku na yai kipi kilitangulia duniani umepatiwa jibu na wanasayansi wa nchini Uingereza ambao wamethibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo mwanzo kabla ya yai.

Kwa kuangalia jinsi ganda la yai lilivyotokea, wanasayansi wa nchini Uingereza wanaamini wamepata jibu la mjadala huo.

Watafiti katika vyuo vikuu vya Sheffield na Warwick nchini Uingereza wamegundua kuwa protini inayoitwa ovocleidin (OC-17) ni muhimu sana katika kutengenezwa kwa gamba la yai.

Lakini protini hiyo hupatikana toka kwenye ovari ya kuku mwenye ujauzito.

Kwa maana hiyo yai lisingekuwepo kama kusingekuwa na protini ambayo inatoka kwa kuku mjamzito.

Watafiti hao waliongeza kuwa protini ya OC-17 husababisha calcium carbonate kwenye mwili wa kuku ibadilike kuwa calcite crystals ambazo ndizo hulifanya gamba gumu la yai ambalo hukilinda kiini cha yai wakati kuku anapoanza kukua ndani ya yai.

Hata hivyo wanasayansi wengine bado hawajaridhika na jibu lililotolewa kuwa kuku ndiye aliyetangulia kabla ya yai.Chanzo:Nifahamishe


Comments

Popular posts from this blog

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE