Mike na Jullie Boyde Siku ya Harusi Usiku wa furaha ya harusi uligeuka kuwa usiku wa majonzi baada ya wanandoa kugundua kuwa hawataweza kuwa na uwezo wa kupata mtoto katika maisha yao ya ndoa kwa kuwa bi harusi ana aleji na mbegu za kiume za mumewe. Mike mwenye umri wa miaka 27 na Julie Boyde mwenye umri wa miaka 26 wakazi wa Ambridge, Pennsylvania nchini Marekani walikuwa katika mapenzi moto moto kwa miaka miwili kabla ya kuamua kufunga ndoa na kuamua kufanya mapenzi bila kutumia kinga kwa mara ya kwanza usiku wa harusi yao. Lakini mambo hayakuenda vizuri kama walivyotarajia kwani ghafla iligundulika kuwa bi harusi alikuwa na aleji na mbegu za kiume za mumewe. Muda mfupi baada ya Mike kuziachia mbegu zake za kiume, Bi harusi alipatwa na maumivu makali sana ambayo mwenyewe anayaelezea kuwa ni sawa na kama mtu alikuwa akipigilia misumari ndani ya mwili wake. Maumivu hayo yaliyoambatana na vipele yaliendelea kwa wiki kadhaa kabla ya kutoweka. Baada ya vipimo kadhaa ...
Comments
Post a Comment