Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta
Timu ya
wachezaji watumishi wa manispaa ya
musoma huenda ikashindwa kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo
serikali za mitaa Tanzania Shimisemta, baada ya wachezaji wa timu hiyo kudai
kuwa hajapewa fedha toka katika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kwenda
kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika huko morogoro.
Wakiongea
kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya watumishi hao wamesema japokuwa
wamekuwa wakitenga muda wao kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na
mashindano hayo lakini wanashindwa kufanya mazoezi kwa uhakika kutokana na
mkurugenzi wa manispaa ya musoma mpaka
kutowathibitishia kwenda kushiriki
katika mashindano huku zikiwa zimebaki siku nne mashindano hayo kuanza.
Wachezaji
hao wamedai kuwa wanashindwa kuelewa toka mwaka 2000 timu ya watumishi wa
manispaa ya musoma haijashiriki katika mashindano hayo kwa kisingizio cha
ufinyu wa bajeti lakini timu za manispaa
ya Musoma vijijini, Bunda, Serengeti pamoja na Tarime zimekuwa zikishiriki
katika mashindano hayo kila mwaka.
Jitihada za
mwanamichezo wetu kumpata mkurugenzi wa manispaa ya musoma kuzungumzia swala
hilo ziligonga ukuta kutokana na kuambiwa yupo nje kikazi.
Comments
Post a Comment