UMUHIMU WA KUANDAA BAJETI KWA MTU, KAYA, FAMILIA, SERIKALI MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI

Ni jambo la kawaida kwa watanzania kutojua umuhimu wa bajeti katika maisha yetu ya kila siku, na tunashindwa kujioji kama mapato yetu yanaendana na matumizi hata katika ngazi ya kaya au familia au mtu mmoja mmoja.

Katika hali ya kawaida tumekuwa na matumizi makubwa kuliko kipato tunachokipata na hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi hawazingatii bajeti wanafikiri bajeti ni kwa ajili ya serikali, makampuni na taasisi wakisahau kuwa mtu anaweza kujiwekea bajeti katika maisha yao ya kila siku.

Leo katika ujasiliamali nahitaji ufahamu kuna umuhimu gani wa kutengeneza bajeti kuanzia ngazi ya mtu, kaya au familia, makampuni makubwa, serikali pamoja na taasisi.

Bajeti: Ni mpango unaonyesha kiasi cha pesa, rasilimali kinachopangiliwa kwa ajili ya kutumika.Kuna aina mbalimbali za bajeti ambazo zinatofautiana kwa tafasiri na utekelezaji.

Ili mtu au taasisi pamoja na serikali iweze kufanikiwa katika maisha ni lazima kutengeneza na kufuata kanuni na kuzingatia mipango utakayoainisha katika bajeti.

UMUHIMU WA BAJETI:

1.Bajeti inatusaidia kukadiria mapato na matumizi

2.Bajeti inasaidia kuangalia mapato halisi yanayoweza kutumika katika shughuli unayokusudia kuifanya

3.Bajeti inatusaida kuangalia uhalisia wa gharama za uendeshaji wa mradi.

4.Bajeti inatusaidia kudhibiti matumizi ya rasilimali.

5.Bajeti inasaidia kutoa hamasa ya motisha kwa wafanyakazi walioko katika kazi/mradi.

6.Bajeti inasaidia kuleta karibu utendaji kazi katika mradi.

Kama unahitaji kufanikiwa katika kazi zako, kufanikisha mradi unaotarajia kuufanya jaribu kuandaa bajeti ambayo itagusa mambo haya muhimu ambayo nimejaribu kuyaainisha hapo juu.

Baadhi ya watu wamekuwa wakiandaa bajeti lakini wamekuwa wakishindwa kuzitekeleza kutokana na kuhamisha pesa toka kwenye kipengele kimoja kwenda kingingine wataalamu wanashauri ni vyema ukaheshimu bajeti uliyotengeneza katika utendaji kazi.

Kwa wale vijana wenzangu ni vyema tukapanga bajeti katika maisha yetu ya kila siku ujue unaingiza shilingi ngapi kwa siku/mwezi na tunatumia shilingi ngapi kwa siku katika ngazi ya familia na je matumizi na mapato yanaendana? kama sio chukua hatua sasa badilika.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE