25 Oct 2014

TIMU ya Polisi Mara imeondoka kuelekea mkoani Shinyanga kucheza mchezo wake wanne dhidi ya timu ya Mwadui huku ikitoa tambo ya kufanya mizuri kwenye mchezo huo kutokana na uelewano wa wachezaji.

Akizungumza kabla ya kuondoka kwa timu hiyo yenye maskani yake mjini musoma Afisa Habari wa timu hiyo Musa Keita amesema timu hiyo inaenda kucheza mchezo wa ugenini ikiwa na pointi 7 ikiwa ni ushindi wa michezo miwili na sare moja katika michezo iliyotangulia imewaweka wachezaji katika ari nzuri ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Amesema kwa sasa kikosi cha timu hiyo kipo kwenye maelewano mazuri uwanjani ndio sababu inayowapa Imani ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa dhidi ya Mwadui hapo kesho.

Keita alisema wanaondoka kwenda kwenye michezo ya ugenini wakiamini kufanya vizuri kuanzia mchezo huo dhidi ya Mwadui kabla ya kuzifuata timu za JKT Kanembwa na polisi ya Tabora na baadae kurudi nyumbani kwenye michezo mingine.

Akizungumzia michezo mitatu iliyotangulia na kujipatia pointi 7,alisema licha ya timu kufanya vizuri lakini pia wanawashukuru wadau wa soka mkoani Mara kuwapa sapoti kwa kila mchezo na kuomba ushirikiano huo uendelee ili timu hiyo iweze kufanya vizuri kwenye michezo mingine.

Katika michezo iliyotangulia Timu ya polisi Mara ilianza kugawana pointi na timu ya Rhino ya Tabora kwa kufungana bao 1-1 kabla ya kushinda 1-0 dhidi ya timu ya Green Worrers ya Dar es salaam na Burkinafaso ya Morogoro.


comments

Post a Comment