AUWAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MISHALE NA KUKATWA MAPANGA WILAYANI TARIME AKIGOMBEA ARDHI

Justus Kamugisha Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi Tarime na Rorya



Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha ng’ereng’ere  wilayani tarime ameuwawa kikatili kwa kuchomwa mishale na kukatwa katwa kwa mapanga .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa kanda maalum ya kipolisi ya Rorya na Tarime Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha  amesema kuwa tukio hilo limetokea jana  majira ya saa mbili asubuhi  ambapo amemtaja aliyeuwawa kwa kuchomwa mishale na mapanga ni Robert  Chacha  kabila mkurya -mkira  44) mkazi  wa kijiji cha Ng’ereng’ere Kata ya Nyamaraga  Tarafa ya Inchugu wilayani Tarime.

Kamugisha amesema kuwa jeshi la polisi linamshikilia juma chacha mwita (22) wa kijiji cha  korotambe  ambaye  amekiri  kufanya hivyo na wenzake saba ambao wamekimbia na polisi wanaendelea kuwatafuta.

Chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kulima katika  eneo linalogombaniwa  na koo hizo ambapo serikali  ilikataza eneo hilo lisitumike kwa shughuli za kilimo ili kuepusha migogoro ya mara kwa mara.

Kamanda  amesema kuwa baada ya Polisi kufika eneo hilo hali ya utulivu  imerejea katika vijiji vya korotambe  kubiterere ambapo kipindi cha miaka mitatu iliyopita kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara baina ya koo mbili za wanchari wakira na waryachoka  kulikuwa kunapelekea  watu kupotea maisha kuchomewa nyumba Maghala ya chakula na chanzo kikubwa ni ardhi na wizi wa Ng’ombe.
                       

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS