MWANACHUO WA CHUO CHA MUSOMA UTALII ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA YA KUMCHOMA VISU MWANACHUO MWENZAKE KISA WIVU WA KIMAPENZI

Mwanachuo wa chuo cha musoma utalii cha mjini Musoma Rose Kanyambo (21),ameshambuliwa kwa kisu mgongoni na ubavuni na mwanachuo mwenzake John Ogolla kutokana na wivu wa mapenzi.

Kwa mujibu wa Taarifa toka kwa mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Mara Irege Ngaregeza, amesema kuwa binti huyo alifikishwa hospitalini hapo siku ya ijumaa Novemba 2 mwaka huu, ambapo binti huyo alikuwa na jeraha la kuchomwa kisu mgongoni na ubavuni na alifikishwa hospitalini hapo akiwa na hali mbaya lakini madaktari walijitahidi kuokoa maisha yake na sasa anaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa taabu wodini binti huyo amesema kuwa siku ya ijumaa majira ya saa mbili asubuhi akiwa chuoni maeneo ya Kamunyonge manispaa ya musomaMwanachuo mwenzake anaefahamika kwa jina John Ogolla alitokea  chuoni hapo na kuanza kumshambulia kwa kumchoma kisu mgongoni mara mbili  na ubavuni ambpo hali hiyo ilimpelekea kutokwa na damu nyingi ambapo alifanikiwa kukimbia hadi alipokuwa anaishi si mbali na chuo lakini kabla hajafika nyumbani alidondoka chini baada ya kuishiwa nguvu  lakini majirani walifanya jitihada za kumpeleka hospitalini.

Binti huyo amewambia waandishi wa habari kuwa chanzo cha tukio hilo la kinyama la kuchomwa kisu ni kumkataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo na mara kwa mara amekuwa akimlazimisha kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini yeye amekuwa akimkatalia.

Baadhi ya majirani na wanachuo ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamesema kuwa  Rose na John wanauhusiano wa kimapenzi kwa  muda mrefu na kijana huyo amekuwa akimsaidia  mambo mengi sana lakini ghafla mpenzi huyo alibadilika na kumkataa bila sababu za msingi hali iliyopelekea kijana huyo kuchukua maamuzi hayo mazito ya kumchoma kisu.

"kabla yaOgolla kutekeleza tukio hilo alikuwa ameandaa barua ambayo ameandika yenye ujumbe uliosomeka ama kufa yeye au rose kanyambo na pia alichukua picha ambayo walipiga pamoja na Rose na kuichora alama ya x kwa kutumia marker pen" alisema shuhuda

Jeshi la polisi linamshikilia john ogolla kuhusiana na tukio na mara baada ya upelelezi kukamilika atapandishwa kizimbani.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS