MREMBO KUTOKA MARA ASHIKA NAFASI YA PILI KATIKA FAINALI ZA REDDS MISS TANZANIA 2012 HONGERA HOMELAND ENTERTAINMENTS

Shindano la kumtafuta Mrembo wa Redds Miss Tanzania 2012 limemalizika siku ya Jumamosi huku mrembo Brigette Alfred kutoka Kitongoji cha Sinza, ameibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Pearl Pub, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam.

Mrembo huyo kutoka kituo cha Sinza na baadaye kuingia katika shindano la Kanda ya Kinondoni, kwa ushindi huo amejitwalia zawadi ya gari aina ya Noah na kitita cha sh milioni 8 zilizotolewa na mdhamini mkuu wa shindano hilo, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.

Mshindi wa pili katika shindano hiloni Eugine Fabian kutoka Mara alijipatia sh milioni 6.2 akifuatiwa na Edda Sylvester kutoka Kitongoji cha Kigamboni, Kanda ya Temeke, aliyeondoka na sh milioni 4.

Nafasi ya nne ilikwenda kwa Magdalena Roy aliyeondoka na sh milioni 3 na Happiness Daniel alishika nafasi ya tano na kujitwalia sh milioni 2.4.

Walishika nafasi ya sita hadi 15, kila mmoja alijinyakulia sh milioni 1.2 na washiriki wengine waliobaki kila mmoja atajipoza kwa sh 700,000.

Kwa ushindi huo, Brigitte ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia, yatakayofanyika mapema mwakani, huku akitegemewa kufanya makubwa zaidi kutokana na maandalizi ya muda mrefu atakayopewa.
Kwa mara ya kwanza katika shindano hilo mwaka huu, warembo watano kati ya 30 waliingia moja kwa moja hatua ya 15 bora, baada ya kutwaa mataji tofauti yaliyokuwa yakiwaniwa na warembo wote 30 kabla ya fainali.

Warembo wengine waliotinga 15 bora ni Babylove Kalala, Mary Frank, Happiness Rweyemamu, Joyce Baluhi, Edda Sylvester, Brigette Fina Revocatus, Catherine Masumbigana, Irene Veda na Eugene Fabian.
Wengine ni Lucy Stephano aliyeshinda Miss Photogenic, Mary Chizi (Miss Sports Lady), Babylove Kalala (Miss Talent), Magdalena Roy (Top Model) na Happiness Daniel aliyetwaa taji la Miss Personality.
Shindano hilo, lilipambwa vilivyo na wasanii Naseeb Abdul ‘Diamond’, Winfrida Josephat ‘Recho’ na kundi la Wanne Star.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE