SIMU BANDIA UGANDA KUZIMWA 2013 TANZANIA, RWANDA NA BURUNDI PIA WAJADILI KUKAMILISHA ZOEZI HILO

Uganda inachukua hatua Sawa na Kenya ambayo ilizima simu za watu zaidi ya Milioni Moja
Uganda imeamua kusitisha mipango yake ya kuzima simu ghushi hadi tarehe moja mwezi Julai mwaka 2013.
Hatua ya serikali inayolenga kuzuia simu bandia kutumika katika mitandao ya simu nchini humo ilikuwa imepangiwa kuafikiwa mwishoni mwa mwezi huu.
Tume ya mawasiliano ya Uganda, imependekeza kuwa takriban asilimia kumi na tatu ya simu milioni kumi na saba za rununu Afrika Mashariki ni ghushi.

Watumiaji wa simu hizo, wana hadi mwezi Machi kuhakikisha kuwa kadi zao zimesajiliwa na tume hiyo.
Pia wametakiwa kubaini nambari yao ya kutambua simu ijulikanayo kama IMEI (International Mobile Equipment Identity) na ambayo huwa ipo kwenye simu halali. Simu ghushi kawaida huwa hazina nambari hii ya utambulisho.

Tume hiyo ya mawasiliano inasema kuwa hatua ya serikali itasaidia maafisa wa sheria kuwasaka wahalifu wanaotumia simu bandia.
Rwanda, Burundi na Tanzania ni miongoni mwa mataifa ya Afrika ambayo yamejadili mipango ya kuzima simu ghushi.

Simu bandia ni maarufu kwa sababu zina bei nafuu kuliko simu halali mara nyingi kwa sababu wanaoziuza huwa wamekwepa kulipa kodi.

Lakini maafisa wanasema kuwa zinaweza kusababisha athari kubwa za kiafya. Wanasema simu hizo hazijafanyiwa utafiti ikiwa ni salama .

Pia wameongeza kuwa simu hizo hazijatengezwa katika njia ambayo inaweza kutumika kwa mitandao ya simu,kwani zinaweza kusababisha simu kukatika mara kwa mara.
chanzo:bbc swahili

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE