MAMLAKA YA MAPATO MKOA WA MARA YAVUKA LENGO KATIKA UKUSANYAJI KODI TOKA MWEZI JULAI HADI OCTOBA 2012

TANZANIA REVENUE AUTHORIRTY              






Mamlaka ya Mapato ya Mkoa wa Mara imevuka  malengo  kwa kukusanya  kiasi cha shilingi bilioni 23. na kuvuka  lengo lililokusudiwa  la shilingi bilioni 22.2 kwa kipindi cha julai hadi oktoba 2012.

Hayo yamesemwa  leo na meneja wa Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mara Joseph Kalinga  wakati akitoa taarifa  ya ukusanyaji wa mapato  kwa mgeni rasmi katibu tawala wa Mkoa wa Mara Clement Lujaji .

Kalinga amesema kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma  yenye  ubora wa hali ya juu na  ya kuvutia  kwa mlipakodi  , idara ya huduma  na elimu  kwa mlipa kodi ,imekuwa  ikitoa semina mbalimbali zenye lengo la kuwaelimisha  walipa kodi sheria  za kodi ,haki za mlipa kodi,wajibu wa mlipa kodi na wajibu wa mamlaka ya mapato imeongeza ushirikiano  baina ya walipa kodi  na watoza  kodi  pamoja  na kuinua  kiwango cha ulipaji  kodi kwa hiari.

Amesema kuwa hali ya makusanyo  kwa mwaka wa fedha wa 2011/12,Mkoa wa Mara ni sawa na asilimia 86 ya lengo lililowekwa hapo awali la kukusanya shilingi bilioni 63.5 kwa kuwa mamlaka imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 54.7

Aidha  kalinga ameelezea changamoto zinazowakabili ni pamoja ongezeko la mahitaji ya mapato  ya serikali katika kutekeleza  mikakati  yake  ya kupambana na umasikini ,ukwepaji kodi kwa kupitia  njia zisizo  rasmi  wakati wa kuingiza  bidhaa nchini  au kutoa bidhaa kwenda nje ya nchi,ukwepaji kodi  kwa njia ya kutotoa risti sambamba na matumizi hafifu ya mashine  za kutolea  risti  EFD) kwa wasiosajiliwa katika kodi ya ongezeko  la thamani  VAT.

Mamlaka kwa kushirikiana  na vyombo vingine  vya uthibiti  ambavyo ni jeshi la polisi ,usalama wa taifa na uhamiaji  vimeweka  mkakati  wa kukabiliana na changamoto  inayohusu  ukwepaji kodi  kwa kutumia njia mbalimbali.

Kwa upande wake mgeni rasmi  katibu tawala wa mkoa wa Mara Clement Lujaji  amesema kuwa dhana ya ulipaji kodi kwa hiari inalenga uelewa wa mlipaji kodi yeye mwenywe na maendeleo ya taifa na jamii nzima ambapo amesema kuwa  kukwepa kodi ni aibu  na sio ujasiri ,hivyo amewataka mamlaka ya mapato kupanua eneo la hamasa kuanzia ngazi ya kata  kwa kuwashirikisha madiwani ili kuongeza walipa kodi, kauli mbiu ulipaji kodi kwa hiari kwa mafanikio ya taifa.

''walipa kodi ni sisi tukilipa  kodi tutaona  zahanati zinajengwa ,shule tra panueni wigo  kutolipa kodi ni aibu'' alisema lujaji.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE