SHILINGI MILIONI 800 ZATUMIKA KUNUNUA VIFAA VYA VILABU 23 VYA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA BARA NA ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara Beldina Nyakeke akipokea sehemu yaVifaa
Jumla ya shilingi milioni 800 zimetumika kununua vifaa vya vilabu 23 vya waandishi wa habari Tanzania bara na zanzibar vilivyoanza  kutolewa jana  na muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa lengo la kuwaongezea ufanisi wa kazi zao ambapo mikoa ya Mwanza ,Mara na Kagera imekuwa ya kwanza kukabidhiwa seti  13 ya vifaa hivyo kila mmoja.
Hafla  hiyo ya makabidhiano ya  vifaa  vya ofisi  za klabu  za waandishi wa habari  Imefanyika  jana katika ofisi za utpc jijini mwanza mtaa wa isamilo ambapo rais wa utpc keneth simbaya  alikabidhi  vifaa  vyenye thamani ya milioni  105 kwa vilabu vitatu vya mwanza,mara na kagera ambapo kila klabu thamani yake ni milioni 35  na kuwataka viongozi  waliopokea vifaa hivyo  kwenda kuvitumia kwa makini  na si kuhoziwa na viongozi  na badala yake  wapange   mipango mikakati itakayowawezesha kujitegemea kwa kubuni miradi endelevu
Awali  Rais   alisema  kuwa UTPC ilianzishwa  kwa madhumuni ya kuimarisha vilabu vya waandishi wa habari nchini ,kuchangia  kuleta maendeleo  ya  taifa sambamba na kuimarisha  demokrasia nchini  .
‘Ili mwandishi wa habari  aweze  kufanya kazi  suala la uhuru ni muhimu sana ,ukibanwa utakuwa katika kipindi kigumu ndicho tunachokipigania utpc alisema simbaya.
Alisema kuwa vifaa hivyo vinalenga kuwa endelevu  katika kazi  ambapo wanahabari watafanya kazi kwa uhuru  na kuhimili matakwa yao ya kila siku tofouti na awali kuwazimu kuazima kwa baadhi ya wadau.
‘Sisi  waandishi wa habari tunadhamana kubwa katika jamii lakini matendo yetu hayaonyeshi taswira nzuri katika jamii ,tuwe mfano  katika jamii ili tuweze  kuwa  kama mhimili wan ne wa serikali  alisema ‘’
Aidha alionya  tabia ya  baadhi ya waandishi wa habari  walioanza kugawanyika kwa kuegemea upande mmoja  badala ya kuwa pande zote kwani kazi ya  mwandishi wa habari kuielimisha jamii  ili kuleta mabadiliko ya nchi kwa kuikomboa jamii inayoteseka  vijijini  na si  kugawanyika  kunakopelekea nchi kufika  pabaya .
Vifaa vilivyokabidhiwa  ni seti 13 kwa kila  vilabu vilivyohudhuria  hafla hiyo kila  klabu imepatiwa  destop computer ,printer ,laptop computer,ups ,binding machine,lamination machine ,photocopy machine ,multimedia  projector,collapsible screen,professional still picture  camera,digital tape recorder,dvd player na tv set.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan  alisema kuwa historia kubwa imetimizwa ya ahadi ikiwa ni mojawapo ya Mkakati wa kuimarisha  vilabu ambayo tayari pia Mafunzo mbalimbali yameshatolewa na utpc nia na madhumuni ni kuwajengea uwezo wanachama wa vilabu ili kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa
Pia amewashukuru wafadhili  kutoka  sida waliowezesha kufanikisha ufadhili huo ,hivyo vilabu havina budi  kutowaangusha  kwa kutumia vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo. 
Wawakiishi wa vilabu hivyo  Wakiwemo wenyeviti wa wawili  kutoka  kagera press club,mwanza press club na katibu wa mara pres club ambaye ni Mjumbe wa bodi ya UTPC  Beldina Nyakeke  wameishukuru utpc kwa msaada huo mkubwa na  wameahidi kuvilinda na kuvitunza vifaa kwani ni sehemu ya maisha yao
Kwa Hisani ya Pasco Michael na Shomari Binda

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE