TIMU YA WAANDISHI WA HABARI YAITANDIKA TRA MARA 2-1 KATIKA MCHEZO WA KIRAFIKI KUELEKEA KUADHIMISHA SIKU YA MLIPA KODI
Benchi la ufundi likifuatilia kwa umakini kambumbu kutoka kushoto ni Emmanuel Almas, George Marato, Shomari Binda,Thomas Dominick na Emmanuel Chibasa |
Kikosi cha Timu ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Mara Kabla ya mechi |
Timu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara Ambayo ilianza kipindi cha Kwanza Katika uwanja wa Posta Musoma Ambapo Timu hiyo iliibuka na ushindi 2-1 |
Timu ya Mamlaka ya mapato ndio walikua wa kwanza kuliona lango la Waandishi wa habari katika kipindi cha kwanza katika mchezo huo ambao ulikua na upinzani mkubwa.
Katika kipindi cha pili timu ya waandishi wa habari ilifanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wako hali iliyozaa mamtunda baada ya timu hiyo kufanikiwa kupata bao kwa njia ya penati kupitia kwa mchezaji wake Paul Peter baada ya mchezaji kufanyiwa madhambi ndani ya 18.
Zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika timu ya waandishi wa habari ilifanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa Alhaj Majogoro na kupelekea mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu ya waandishi wa habari 2 na timu ya mamlaka ya mapato mkoa wa mara 1.
Timu ya waandhi wa habari imekabidhiwa kombe leo katika kilele cha siku ya mlipa kodi sherehe ambazo zimefanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mkendo.
Comments
Post a Comment