MUSOMA YAPATA MABILIONI TOKA BENKI YA DUNIA KUTEKELEZA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO MUSOMA MJINI


HALMASHAURI ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara, imepata msaada wa zaidi ya sh bilioni 21 kutoka Benki ya Dunia (WB).

Fedha hizo zitaanza kutolewa Julai mwaka 2013 na zitatolewa kwa miaka mitatu ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Musoma mjini.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma, Alex Kisurura, alisema hayo jana mjini hapa alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu mipango ya maendeleo kwa wakazi wa mji huo na kujinasibu kwamba katika kipindi cha miaka mitano manispaa hiyo itafurahia mafanikio ya kisekta.

Kwa mujibu wa mstahiki huyo fedha hizo za ufadhili wa Benki ya Dunia zimelenga kutekeleza miradi ya kiuchumi ikiwemo miundombinu ambapo kila mwaka benki hiyo itatenga fedha ili kufikia malengo ya maendeleo.

“Manispaa ya Musoma tumekubaliwa na Benki ya Dunia kupewa dola milioni 14.1 za Marekani kuanzia Julai 2013 na tutapewa kwa awamu tatu kila mwaka wa fedha!

“…Licha ya Benki ya Dunia kutupa fedha hizi imetupa masharti ya kuhakikisha matumizi yake yanakuwa ya wazi, ukusanyaji wa mapato uwe mzuri. Ufadhili huu utaishia mwaka 2018; naamini muda huo Musoma itakuwa mbali kimaendeleo,” alisema meya huyo.

Hata hivyo, alizitaja halmashauri za Geita, Bariadi, Manispaa ya Bukoba na Shinyanga kuwa ni miongoni mwa halmashauri zilizoomba na kupewa ufadhili wa aina hiyo lakini manispaa yake imepata fedha nyingi zaidi kwa ukanda wa Ziwa Victoria.
Chanzo: Tanzania Daima

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS