AMSHITAKI MKEWE BAADA YA KUZAA MTOTO MWENYE SURA MBAYA, ASHINDA KESI ALIPWA MAMILIONI YA PESA

Hii ndo Picha ya Mwanamke huyo anaonekana kabla na baada ya kufanyiwa Oparesheni

Mwanaume mmoja nchini China alishtuka baada ya mkewe kuzaa mtoto mwenye sura mbaya na aliamua kumfikisha mkewe mahakamani kwa kutomjulisha kuwa sura yake nzuri ilitokana na operesheni za kubadilisha sura, alishinda kesi na kuzawadia fidia ya mamilioni.


Wakati Jian Feng alipomuona mtoto wake mchanga kwa mara ya kwanza alishtuka sana.

Mtoto wake huyo wa kike alikuwa na sura mbaya kiasi cha kwamba alishindwa kuamini kuwa mkewe aliyekuwa akionekana mrembo sana angeweza kuzaa mtoto kama huyo.

Jian alimgeuzia kibao mkewe na kumshtumu kuwa aliisaliti ndoa yao na kufanya mapenzi nje ya ndoa yaliyopelekea kuzaliwa kwa mtoto huyo.

Baada ya hali kuwa tata, mkewe alilazimika kutoboa siri kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni zilizomgharimu zaidi ya dola 100,000 ili kuirekebisha sura yake aonekane mrembo. Mkewe alisisitiza kuwa mtoto huyo ni wa kwao.

Jian alikasirika sana kusikia hivyo na kuamua kumfikisha mkewe mahakamani akidai kuwa alirubuniwa kuingia kwenye ndoa na alidai fidia ya mamilioni ya pesa.

"Nilimuoa mke wangu kwa mapenzi makubwa kwa jinsi alivyokuwa akionekana lakini punde baada ya kufanikiwa kupata mtoto wa kwanza matatizo yalianza kwenye ndoa yetu", alisema Jian.

"Binti yetu alikuwa na sura mbaya sana kiasi cha kwamba nilitishika sana", Jian aliwaambia wanasheria wake kuwa mkewe alimvuta kwenye ndoa kwa kufanya operesheni ya kutengeneza sura yake aonekane mrembo na kuzaliwa kwa mtoto wao huyo ndiko kulikopelekea ukweli kujulikana.

Mahakama ilikubaliana na madai ya Jian na kuamua alipwe fidia ya dola 120,000 ( zaidi ya Tsh. milioni 170) baada ya mkewe kukiri kuwa hakuwahi kumwambia mumewe kuwa urembo wa sura yake unatokana na operesheni.

Mahakama ilimuona mkewe ana hatia ya kumrubuni Jian kuingia kwenye ndoa na ilikubali maombi ya Jian ya kuivunja ndoa hiyo.Chanzo:Nifahamishe
  

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE