JESHI LA POLISI MKOANI MARA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA YA KUMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Absalom Mwakyoma Watu watatu wakazi wa kijiji cha motukeri katika wilaya ya Serengeti Mkoani Mara,akiwemo raia wa nchi ya Kenya wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukamatwa na bunduki aina ya smg Fn na risasi 96 kinyume cha sheria. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara kamishina msaidizi Absalom mwakyoma amethibitisha kukamatwa kwa watu hao ambao amewataja kuwa ni sabasaba makuru kambarage (31),Timothy Bernad omoke (20) raia wa Kenya na pius mayengo sengeka( 43) wote wakiwa wakazi wa kijiji hicho kilicho kata ya nata wilayani Serengeti. Kamanda Mwakyoma amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa octoba 23 majira ya saa mbili na nusu usiku mwaka huu katika kitongoji cha mageriga nyumbani kwa mtuhumiwa wa kwanza sabasaba wakimiliki silaha hiyo ya kivita kinyume cha sheria Amesema kuwa Maafisa wa polisi wakishirikiana na maafisa wa shirika la hifadhi Taifa (TANAPA)siku ya tukio baada