Mfahamu Mwalimu Mlemavu wa Mikono Anayefundisha Kwa Kutumia Miguu

Mwalimu Akitumia Mguu Kuandika


Mwanamke wa nchini Marekani ambaye alizaliwa akiwa hana mikono ameonyesha changamoto kwa watu kwasababu ya vilema vyao hawawezi kufanya chochote kwa kuweza kuajiriwa kazi ya ualimu akifundisha wanafunzi kwa kuandika ubaoni kwa kutumia miguu yake.


Mary Gannon, amejiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi kwenye shule ya Lakewood iliyopo Ohio nchini Marekani.

Tofauti na walimu wenzake, Mary anatumia miguu kuandika ubaoni na pia anatumia miguu kuandaa ripoti kwenye computer akitumia vidole vya miguu yake kuandika kwa kutumia keyboard ya kompyuta yake ya ofisini.

Mwalimu Mary ambaye hufundisha somo la hisabati na sayansi alizaliwa nchini Mexico akiwa hana mikono na alilewa kwenye kituo cha kulea yatima mpaka familia moja ya nchini Marekani ilipojitolea kumchukua na kumlea.

Mary alianza kazi kwenye shule hiyo mwaka jana kama mwalimu wa akiba lakini hivi sasa amejiriwa kabisa akifundisha wanafunzi wa darasa la saba na la nane,

Mbali ya kutumia miguu yake kufundishia, Mary pia anaendesha gari lake kwa kutumia miguu.


 Ni vyema jamii ikawapa nafasi watu wenye ulemavu kujishughulisha katika jamii pia hapa nchini Tanzania pia tunaitaji kuwaona walemavu wakiajiliwa katika kazi mbalimbali, huduma zinaboreshwa kama vile Vyoo, Huduma za Kibenki, Usafiri na pia Elimu.Kwa hapa Musoma Elimu kwa watu wenye ulemavu inatolewa pale Lake Victoria Disability Centre jirani na Tanesco.

Chanzo: Nifahamishe

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE