Uwanja wa ndege Mwanza |
KIKAO Cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mara imeutaka Mkoa wa Mwanza
kuacha kabisa mchakato wa kubadilisha jina la Uwanja wa Ndege wa
Mwanza na Kuitwa jina la Serengeti International Airport.
Mjadala huo uliibuka hivi karibuni katika kikao cha kamati ya Ushauri
ya Mkoa huo ambapo lilijadiliwa na kutaka kuita jina hilo katika
uwanja wao wa ndege wa kimataifa wa mkoa huo.
Baada ya kupata taarifa hiyo wajumbe wa kikao hicho waliamaki na kwa
sauti moja wameutaka mkoa wa Mwanza kuacha mara moja nia ya kulitumia
jina hilo na kuwataka watumie majina mengine kama vile la Victoria au
sangara.
Kauli hiyo ilipitishwa na wajumbe wa Kikao cha Ushauri wa Mkoa huo
baada ya kupitia taarifa ya ujenzi wa Uwanja wa Kisasa kutoka kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Kimulika Galikunga
ambapo alisema kuwa Halmashauri hiyo imeshampata mwekezaji ambaye
atajenga uwanja huo na kutumia jina hilo.
“Tayari tumempata mmoja wa wawekezaji ambaye ni wa kampuni ya Grumeti
Reserves ambaye aliomba kibali Serikalini cha kuweza kufanya biashara
pamoja na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa na kupata kibali
hicho mwaka 2006 na amweweka wazi kuwa atatekeleza ahadi hizo,”alisema
Galikunga.
Alisema kuwa shughuli za awaloi za zilishafanyika kwa kugharimiwa na
kampuni hiyo ni pamoja na kuhamisha wakazi waliokuwa karibu na eneo la
mradi huo ambapo jumla ya shilingi Milioni 400 walilipwa wakazi hao,
pamoja na kuhamishwa kwa shule ya msingi Burunga iliyopo karibu na
mradi.
“Upimaji wa eneo linalokusudiwa ulifanyika na kuwekewa mpaka na hivyo
kutambulika rasmi kuwa ni eneo maalumu kwa ajili ya mradi huo, na hati
miliki ya ardhi ilitolewa,”alisema.
Chanzo: Thomas Dominick, Musoma
Comments
Post a Comment