MREMBO KUTOKA MARA ATINGA FAINALI ZA REDD'S MISS TANZANIA



 Mkoa wa Mara umeendelea Kufanya vyema katika mashindano ya ulimbwende mwaka huu baada ya mwakilishi wa mkoa kufanya vyema tena na kuingia katika fainali zashindano la Urembo la Redd's Miss Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwa bwana Godsos Mukama ambaye ndie mwandaji wa shindano la Miss Mara kupitia kampuni yake ya Homeland Entertainment amesema mrembo kutoka Mkoani Mara ambaye pia anashikilia Taji la Urembo Kanda ya Ziwa (Miss Lake Zone) amefanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye Fainali za Shindano la Urembo (Redd's Miss Tanzania) Baada ya kuteuliwa kuwa Balozi Naura Spring Hotel
 
katika Shindano dogo la kumtafuta Top Model lililofanyika usiku wa siku ya Jumamosi Jijini Arusha katika Hotel ya Naura Spring. Eugenia pia ni Balozi wa Barrick North Mara Kampuni inayojishughulisha na Uchimbaji wa Dhahabu Mkoani Mara.
 
 
 
 

Huyu ndie Bwana Godsos Mukama ambaye kwa miaka yote amekua akiandaa mashindano ya Miss Mara na kuwatoa washiriki mpaka ngazi ya Taifa. Hapa akiwa katika mapumziko aki show love!


Tuna imani mwanadada huyu atafanya vyema katika ngazi ya Taifa na mkoa wa Mara Tuweze kuandika Historia kwa Mara ya kwanza kutwaa taji la miss Tanzania.


Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS