USALITI WA MAPENZI WASABABISHA MWANAUME KUKATWA NYETI







 Hudaiwa kuwa hakuna mtu mwenye hasira kali kama mwanamke anayegundua kuwa mumewe ana kimada nje, hayo yalijidhihirisha nchini Peru pale mwanamke mmoja nchini humo alipoukata uume wa mumewe wakati akiwa amelala na kisha kuutupa uume huo chooni. Mwanamama Huaman Julia Muñoz mwenye umri wa miaka 41 anashikiliwa na polisi baada ya kulipiza kisasi cha mumewe kutembea na kimada nje kwa kuukata uume wake.

Julia alienda na mumewe hotelini kwenye mji wa Brena nchini Peru na wakati mumewe akiwa amepitiwa na usingizi, Julia alitumia kisu kikali cha jikoni kuukata uume wa mumewe na kisha alikichukua kipande cha uume huo na kukitupa chooni na kukiflash.

Haijajulikana kama Julia alimwekea kilevi kilichomlalaza mumewe fofofo kabla ya kutimiza lengo lake hilo la kuyanyofoa maeneo ya kujidai ya mumewe.

Julia alijaribu kukimbia kutoka kwenye hoteli hiyo lakini kelele za mumewe zilifanya wahudumu wa hoteli hiyo wamkamate na kumfikisha polisi.

Julia alikiri mbele ya polisi kuwa aligundua kuwa mumewe alikuwa akimsaliti kwa kutembea na mwanamke mwingine nje na hasira alizokuwa nazo ndizo zilizopelekea achukue uamuzi huo wa kuukata uume wa mumewe.

Julia anashikiliwa na polisi wakati mumewe amelazwa hospitali kwenye chumba cha watu mahututi hali yake ikiwa mbaya sana.

Hii sio mara ya kwanza tukio kama hili kutokea duniani, mwezi mei mwaka jana, mwanamke mmoja wa nchini Bangladesh aliukata uume wa mwanaume aliyekuwa akijaribu kumbaka na kisha kukichukua kipande cha uume huo na kukipeleka polisi kama ushahidi.

Kesi inayojulikana sana ni ile ya mwezi julai mwaka jana nchini Marekani ambapo Catherine Kieu wa California, alimdanganya mumewe kuwa anataka kujaribu staili tofauti ya mapenzi na kisha kuifunga mikono na miguu ya mumewe kwenye kitanda kabla ya kuukata uume wake kwa kutumia kisu kikubwa chenye ncha kali.

Kama haitoshi, mwanamke huyo ili kuhakikisha madaktari hawataweza kukiunganisha kipande hicho alikichukua kipande hicho cha uume wa mumewe na kukisaga kwenye mashine ya kusaga taka za majumbani.

Catherine alikamatwa na kutupwa jela ambapo kesi yake inaendelea akiwa jela baada ya kushindwa kulipa dhamana ya dola milioni moja. Mumewe alifariki dunia kufuatia shambulio hilo.


Chanzo: nifahamishe

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS