JESHI LA POLISI MKOANI MARA LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA YA KUMILIKI SILAHA KINYUME NA SHERIA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishina Msaidizi Absalom Mwakyoma
Watu watatu wakazi wa kijiji cha motukeri katika wilaya ya
Serengeti Mkoani Mara,akiwemo raia wa nchi ya Kenya wanashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma za kukamatwa na
bunduki aina ya smg Fn na risasi 96 kinyume cha sheria.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara kamishina msaidizi Absalom mwakyoma amethibitisha kukamatwa kwa
watu hao ambao amewataja kuwa ni sabasaba makuru kambarage (31),Timothy Bernad
omoke (20) raia wa Kenya na pius mayengo sengeka( 43) wote wakiwa wakazi wa
kijiji hicho kilicho kata ya nata wilayani Serengeti.
Kamanda Mwakyoma amesema kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa octoba 23
majira ya saa mbili na nusu usiku mwaka huu katika kitongoji cha
mageriga nyumbani kwa mtuhumiwa wa kwanza sabasaba wakimiliki silaha hiyo ya
kivita kinyume cha sheria
Amesema kuwa Maafisa wa polisi wakishirikiana
na maafisa wa shirika la hifadhi Taifa (TANAPA)siku ya tukio baada ya kupata
taarifa kutoka kwa raia wema walifanya msako na kufanikiwa kuwakamata
watuhumiwa hao wakiwa na vipande 10 vya nyama kavu ya
pori ,mikia sita ya nyumbu na mayai mawili na maganda mawili ya mayai ya
mbuni kinyume cha sheria ambapo thamani ya nyara hizo hajafahamika.
“ Polisi wakiwa katika msako mkali
wa kuwasaka wahutumiwa hao walifika kijijini hapo majira ya saa mbili na nusu
usiku ndipo waliwakuta ndani ya nyumba hiyo walimokuwa wakihifadhi nyara hizo
na kisha kufanikiwa kuwakamata”alisema kamanda mwakyoma.
Inadaiwa kuwa bunduki hiyo imekuwa
ikitumika kuulia wanyama pori na wakati mwingine vitendo vya uharifu sehemu
mbalimbali hapa nchini na kuhatarisha usalama
na maisha ya wananchi pamoja na mali zao.
Kamanda alisema kuwa upelelezi utakapo kamilika watuhumiwa
watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria na ametoa wito kwa wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi
kufichua na kuwataja waharifu.
Comments
Post a Comment