JINSI YA KUPATA MTAJI NA NAMNA YA KUTUMIA MTAJI KATIKA BIASHARA
JINSI YA KUPATA MTAJI NA NAMNA YA KUTUMIA MTAJI KATIKA BIASHARA
MTAJI
Mtaji ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha kitu
kingine kwa lengo la kupata faida.Biashara oyote iwayo lazima ianze na
mtaji. Kuna aina tano za mitaji kama ifuatavyo:-
1. Mtaji wa fedha( financial capital)
2. binadamu mwenyewe( human capital) vitu kama ujuzi, elimu na kufanya kazi kwa bidii.
3. Jamii ( social network capital) ushirikiano na watu wengine katika biashara
4. utamaduni halisi wa mjasiliamali- utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii,historia ya familia
5. fani au utaalamu katika jambo flani
JINSI YA KUPATA MTAJI.
hapa tunaangalia vyanzo vya mtaji kwa mjasiliamali. Wajasiliamali wengi
wanapata changamoto kubwa katika kupata mitaji ya kuanzishia biashara.
nivigumu kuanzisha biashara bila kuwa na mtaji wa kutosha,hivyo basi
mtaji ni muhimu sana lakini mtaji pekeyake hautoshi kuanzisha biashara
ni lazima uwe na elimu ya ujasiliamali ili uweze kufanikiwa katika
biashara. kuna njia mbalimbali za kupata mtaji na njia hizo
zimegawanyika katika mafungu mawili ambayo ni chanzo cha ndani na chanzo
cha nje.
Chanzo cha ndani ( internal sources of capital)
1. Mtaji toka kwa mjasiliamali mwenyewe. huu ni mtaji ambao
mjasiliamali anakuwanao kabla hajaanza biashara. huu ni mtaji bora sana
kwani humilikiwa na mjasiliamali mwenyewe na hatakiwi kurudisha rejesho
hata baada ya kupata faida.
2. Mtaji ambao unapatikana wakati biashara injiendesha. faida
inayopatikana katika biashara inaweza kutumika kama mtaji. njia hii ndio
huchangia kukua kwa biashara.
3. hisa. baadhi yawajasiliamali wanaweza kuamua kuwekeza katika hisa za
makampuni. uwekezaji katika hisa husaidia kupata mtaji pale ambapo
kampuni litagawa faida kwa wanachama waliowekeza katika hisa. pia
mjasiliamali anaweza kupata mtaji kwa kuuza hisa kwa mtu mwingine au
muwekezaji wa nje.
chanzo cha nje ( external sources of capital)
hapa tunaangalia mtajia ambao mjasiliamali anaweza kuupata toka nje ya
yeye mwenyewe. baadhi ya vyanzo hivyo ni kama ifuatavyo.
1. mkopo toka benki
huu ni mkopo ambao ulipaji wake ni wa muda mrefu.viwango vyariba si
vikubwa sana ambavyo mjasiliamali anaweza kumudu kulipa endapo biashara
itafanikiwa. mikopo ya benki inahitaji dhamana ya vitu visivyo hamishika
mfano nyumba, shamba nk.
Chanzo:gjob.blogspot.com
Comments
Post a Comment