ZIFAHAMU NJIA ZA KUPATA MTAJI WA BIASHARA

Njia za kupata Mtaji wa biashara: Baada ya kuamua kuingia katika ujasiriamali, sasa unahitaji mtaji wakufanyia na kukuzia biashara yako. Swali, wapi utapata huo mtaji nk. Mlolongo huu hapa chini utakusaidia kujua ni wapi utapata huo mtaji wa biashara.
Mali binafsi
    1. Shamba, fedha, nyumba, gari, mifugo, mazao nk
    2. Mkopo:-
Mkopo kutoka kwa:
  1. Marafiki, ndugu, jamaa, serikali
  2. Taasisi za kukopesha kama pride, seda, faida, best, finca
  3. Benki nk.
a) Masharti ya mkopo
- Dhamana kama vile nyumba, arthi, mazao, kikundi n.k.
- Mchanganuo wa biashara
- Biashara inayo endelea(<miaka 3)
- Kuwepo kwa ofisi kama ni mkopo mkubwa zaidi ya milioni 3
- Biashara iliyosajiliwa kam ni biashara kubwa
- Riba ya mkopo
- Kiasi cha mkopo na uwezo wa mkopo
- Muda wa kurudisha mkopo na riba
Vyanzo vya kukopa mabenki, mashirika binafsi Kama vile SEDA, PRIDE, FINCA n.k
  1. Kibati ; mfano, Mtaji ni unaotakiwa ni ni Tshs100,000 watu 10 mnaweza kuzungusha 10,000 miongoni mwenu kila mwezi, kila mtu atapata mtaji wa Tshs100,000 ndani ya mwaka.
  2. SACCOS( chama cha kuweka na kukopa)
  3. Kudunduliza ( banki ya kopo). Mfano; Mtu moja aliyekuwa mlevi alikuwa akitumia Tshs 5,000 kila siku kunywa pombe. Alikata shauri ya kuacha pombe na kudunduliza Tshs 5,000 kila siku kwa muda wa mwaka 1 na akaweza kujenga nyumba ya kisasa yenye vyumba 2 na sebule.
  4. Kuafanya harambee (fund raising)
  5. Kuuza hisa
  6. Msaada kutoka mashirika yasiyo ya kiserkali, watu binafsi, mashirika binafsi na taasisi za kiraia

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE