MWANAUME MMOJA WILAYANI BUNDA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA YA KUMTOROSHA MWANAFUNZI NA KUMZALISHA WATOTO WAWILI
MWANAUME mmoja anayetuhumiwa kutorosha
mwanafunzi wa shule ya sekondari Kibara, iliyoko wilayani Bunda, mkoani Mara,
kwa zaidi ya miaka mitatu, amekamatwa na kufikishwa katika mahakama ya wilaya
ya Bunda, akiwa tayari amekwishamzalisha mwanafunzi huyo watoto wawili.
Mwanaume huyo Joel Joseph, amekamtwa juzi
mjini Musoma, wakati akiwa ndani ya daradara baada ya kuwekea mtego na mzazi wa
mwanafunzi huyo, mwalimu Eward Masatu.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kumtorosha
mwanafunzi huyo aitwaye Nyafwele Edward au Edina Edward, aliyekuwa anasoma
kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kibara, na kuishi naye kama mke wake,
tangu mwaka 2009.
Imeelezwa kuwa Novemba 18, 2009 mtuhumiwa
pamoja na mwanafunzi huyo, wote walikamatwa na kufikishwa katika kituo kidogo
cha polisi Kibara, lakini kesho yake wakatoroka katika mazingira ya kutatanisha
na kwamba walikuwa wakiishi katika miji mbalimbali ikiwemo Musoma, Tarime,
Mwanza na Kahama.
Mwalimu Masatu amesema kuwa kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo kumetokana na mtego wake aliouweka, baada ya mtoto wake kupata
ujauzito wa pili na kurejea nyumbani kwao kwa ajili ya kujifungua huku
akimuomba mzazi wake amsamee.
Amesema kuwa baada ya binti yake kumuomba
radhi alimkubalia na baada ya kujifungua walianza kumfuatilia mwanaume huyo,
ambapo juzi alikamatwa na jana akafikisha katika mahakama ya wilaya ya Bunda,
mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Safina Simfukwe.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Bw.
Masuod Mohamed, baada ya kumsomea mashitaka yake, mtuhumiwa huyo alikana na
amepewa dhamana baada ya kudhaminiwa na watu wawili, ambapo kesi yake itatajwa
tena novemba 16, mwaka huu.
Chanzo:Ahmed makongo, Bunda
Comments
Post a Comment