TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS

comments
ikafika muda tozi na sinyorita wakapiga mavazi kivingine
makamuzi ya tozi yanaendelea
Hapa nikitoa maelekezo kwa watoto kuondoka make muda wao ulikua umekwisha
Hapa ni sehemu ya jikoni na Albert hapa anaweka order ya mchemsho siku ya krismac
Wadau wa The Track Master walifika asubuhi kutoa sapoti wakati wa maandalizi kutoka kulia ni mshikaji wetu ALBET wa vodacom akiwa na fans wetu wengine Denis wa muwasa mwenye shati jeupe
Viunga tofauti tofauti ambavyo vimedizainiwa kwa ubunifu wa hali ya juu pale bwalo
Hii ndio Kaunta ya nje ambayo inatumika kwa sasa
Haya ndio mandhari halisi ya ufukwe wa bwalo la polisi yani kumetulia sana ebu fika pale upate huduma safi ya vinywaji na chakula kwa bei poa kabisa
Nyomi ilikua ya kutosha katika ufukwe wa bwalo la polisi mwisenge eneo lote lilijaa watu balaaa usichezee The Track Masters Djs weweeeeeeeeeeeeeee
Watoto walikuja kwa wingi sana bwalo la polisi hii ni kudhirisha kuwa tozi gamba ndio habari ya mjini hakuna cha nani wala nani
Tozi Gamba a.k.a Mtoto wa Mama Mzigo akikamua Show ya mchana pale Bwalo la Polisi Mwisenge siku ya Christmas
Tozi Gamba akiwa na Sinyorita wakati wa makamuzi ya mtoto wa mama mzingo kila kitu kilo

KONTENA LA KONDOMU FEKI LAKAMATWA BANDALINI JIJINI DAR ES SALAAM

comments
Kondomu
KONTENA lililosheheni kondomu za kiume kutoka nchini India imekamatwa na kuzuiliwa katika Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wamelazimika kufanya msako mkali kwenye baadhi ya maduka ya dawa jijini Dar es Salaam baada ya kubainika kwamba tayari kondomu hizo zipo sokoni.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Leandri Kinabo alizitaja kondomu hizo kuwa ni aina ya Melt Me zenye thamani ya Sh222.1   milioni zilizokamatwa tangu Oktoba 23 mwaka huu na kuzuiliwa bandarini hapo kwa taratibu zaidi za kisheria.

“Jambo lililotushtua ni kwamba zimebainika kwamba zipo madukani, tukajaribu kufuatilia tena bandarini tukifikiri kuwa huenda zimetolewa kinyemela licha ya kuzuiliwa ili ziteketezwe au zirejeshwe nchini India kwa gharama zao wahusika.

Tulipokwenda bandarini tukabaini kwamba bado zipo katika hali ile ile, kumbe  zimeingizwa nchini kwa njia ya panya, kwa kweli ni mbovu na ndiyo maana tumelazimika kuwajulisha wanahabari ili muwape taarifa wananchi wawe makini,” alisema Kinabo.

Alifafanua zaidi kwamba kondomu hizo ni mbovu kwani zimebainika kuwa na vitundu, pia zinapasuka haraka, hazina kabisa viwango vya ubora wa bidhaa unaotakiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO).
Kinabo alisema kuwa TBS bado wanaendelea kufanya mawasiliano na kampuni iliyotengeneza kondomu hizo, lakini kwenye kasha  lake inaonyesha kuwa inaingizwa nchini na kampuni ya Fair Deal Exim ya Dar es Salaam.   Chanzo Gazeti la Mwananchi

HOSPITALI YA MKOA WA MARA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA BAADHI YA DAWA

comments
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Iragi Ngerageza
Hospitali ya Mkoa wa Mara inakabiliwa na upungufu wa baadhi ya dawa zinazotolewa na bohari ya dawa (msd) hali inayopelekea dawa zinazokosekana kununuliwa kwenye maduka binafsi yaliyoteuliwa na serikali.

Akiongea na chibasa blogspot mganga mfawidhi w badoa hospitali hiyo Iragi Ngerageza amesema kuwa bohari ya dawa imekuwa ikiwapa dawa ambazo hazitoshelezi mahitaji ya hospitali hiyo.

Amesema kuwa hivi karibuni hospitali hiyo imenunua dawa kwenye bohari ya dawa zenye thamani ya shilingi 41,190,100 lakini bado kuna mahitaji ya baadhi ya dawa hali inayosababisha wananchi kwenda kununua madawa kwenye maduka ya mitaani.

Katika kukabiliana na tatizo hilo tayari uongozi wa hospitali kupitia kamati yake inafanya jitahada ya kununua dawa ambazo hawakuzipata kutoka bohari ya dawa (msd) kwenda kununua dawa hizo kwenye maduka ya watu binafsi ambayo yameteuliwa na serikali.

“Wananchi wanatakiwa kuelewa kuwa tunaupungufu wa baadhi ya dawa lakini tunafanya jitahada za kununua dawa hizo ili kuwawezesha wananchi kupata dawa hizo” alisema


Ili kukabiliana na changamoto hiyo ameiomba serikali kuiwezesha bohari ya dawa kutoa dawa kulingana na mahitaji husika ili kuboresha huduma ya afya kwa jamii hususani wale wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hiyo.

KIPIMO CHA X-RAY KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MARA KIMEFANYIWA MATENGENEZO

comments
MGANGA MFAWIDHI WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA IRAGI NGERAGEZA AKITOA MAELEZO KWA BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI.

BAADHI YA WAANDHI WA HABARI MKOANI MARA WAKIWA NA MGANGA MFAWIDI WA HOSPITALI YA MKOA WA MARA KUTOKA KUSHOTO NI HELLEN MAGABE, IRAGI NGERAGEZA AMBAYE NDIE MGANGA MFAWIDHI, EMMANUEL CHIBASA NA LAZARO KAAJI


Baadhi ya wagonjwa wanaokwenda hospitali ya Mkoa wa Mara kupima kipimo cha X-ray wamelalamikia uongozi wa hospitali hiyo kutotoa taarifa kwa wagonjwa baada ya kukosekana kwa huduma hiyo kwa muda.

Wakiongea na gazeti hili leo wakiwa nje ya chumba cha x-ray mmoja wa wagonjwa Bi Mage Hilary amesema toka siku ya jumatatu amekuwa akiwahi kila siku asubuhi ili kupata huduma hiyo lakini ameshindwa kuipata na hakuna taarifa yoyote toka kwa daktari kwa nini hataki kuwahudumia.

“Ndugu mwandishi hii sio haki kabisa we fikiria toka asubuhi tuko hapa na hakuna taarifa yoyote toka kwa daktari kwanini huduma haitolewi tunawaona tu madaktari wanapita hapa wanatuona kama majengo je hii ni haki kweli” alisema bi Mage.

Naye Piter Majaliwa mkazi wa kigera manispaa ya musoma amesema kuwa kwa muda wa wiki moja amekuwa akifika hospitalini hapo kupata huduma hiyo baada ya kupata ajali ya pikipiki na kuumia ubavu wa kushoto lakini kila anapofika hapati huduma na hivyo anashindwa kuelewa tatizo ni nini kwani hakuna taarifa iliyotolewa kwao ili wajue nini cha kufanya.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa huduma ya x-ray katika hospitali hiyo ilikuwa haipatikani kwa muda wa wiki mbili kutokana na mashine kuharibika ghafla.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Iragi Ngerageza amesema kuwa mashine ya x-ray iliharibika ghafla wiki mbili zilizopita na walikuwa wanawasubiri mafundi kutoka kampuni ya Philips ambayo ndio walipewa tenda ya kufunga na kutengeneza mashine hiyo.

Amesema baada ya tatizo hilo kutokea walishindwa kuchukua mafundi sehemu nyingine kwa ajili ya kuitengeneza kwani tayari walishaweka makubaliano na kampuni ya Philips kuwa wao ndio watakua wanaifanyia matengenezo mashine hiyo, na kilichosababisha mashine hiyo kuharibika ni kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu.

Ameongeza kuwa uongozi wa hospitali hiyo umejitahidi kulishughulikia tatizo hilo na tayari wamefanikiwa kurejesha huduma hiyo lakini changamoto inayowabili pia ni uchache wa madakitari na wauguzi katika kutoa hudumia.

Aidha amesema kuwa changamoto nyingine inayowakabili ni fedha ambapo ili hospitali iweze kuendesha shuguli zake kwa ufasaha inahitaji shilingi milioni ishirini na sita(26) kwa mwezi lakini wamekuwa wakishindwa kufikia lengo hilo kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na swala la rushwa lakini kwa sasa wanatarajia kufikisha lengo la kukusanya kiasi hicho cha pesa ama zaidi baada ya kufanya kazi na watu kutoka taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa takukuru.

UTAFITI WA WANASAYANSI WAONYESHA TUNDA LA TIKITI MAJI LINASAIDIA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME

comments
T
Watafiti wa nchini Marekani wamegundua kwamba matikiti maji yanaongeza nguvu za kiume na yanasaidia kutoa tiba kwa wanaume wenye upungufu wa nguvu za kiume.
  
Watafiti katika chuo kikuu cha Texas A&M wamegundua kwamba matikiti maji yanaweza yakatumika kama "Viagra ya Asili" kwa wanaume wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.

Watafiti hao walisema kuwa tikiti maji lina amino acid nyingi za citrulline ambazo huifanya mishipa ya damu itanuke na iwe katika hali kama ile ambayo mtu anayetumia viagra au madawa ya kuongeza nguvu za kiume huwa nayo.

Citrulline ikiwa mwilini hugeuka kuwa "arginine" mojawapo ya aina za amino acid. Hali hii husababisha kuongezeka kwa kiwango cha nitric oxide kwenye damu. Nitric oxide husaidia kuifanya mishipa ya damu itanuke.

Hata hivyo watafiti hao hawakuweka wazi idadi ya matikiti maji ambayo mwanaume anatakiwa kula ili aweze kuwa na nguvu za kiume kama za viagra.

Bhimu Patil, mkurugenzi wa maabara iliyofanya utafiti huo alisisitiza kuwa ulaji wa tikiti maji wa mara kwa mara unasaidia kuzuia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mojawapo ya faida nyingine ya tikiti maji iliyotajwa ni kusaidia kushusha shinikizo la damu.chanzo nifahamishe

MBUNGE WA MUSOMA MJINI VICENTI NYERERE ASEMA BULEMBO AMEINGIZWA MJINI

comments
VICENTI NYERERE MBUNGE WA MUSOMA MJINI
MBUNGE wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), amekana kumtambua mtu aliyejinadi alikuwa Meneja wa Kampeni wa jimbo hilo, Juma Songo, ambaye amejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema chama hicho kimetapeliwa.

Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Nyerere alisema aliyekuwa meneja kampeni wake ni Fikiri Malenge, ambaye mpaka sasa ni katibu wake na wala si Songo.

Nyerere alisema Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa CCM, Abdallah Bulembo, amekutana na watoto wa mjini na kumdanganya, naye akajikuta anadanganyika kama mtoto mdogo.
“Bulembo hakujua kama Musoma kuna watoto wa mjini, sasa kaingizwa chaka bovu naye kaingilika kwa kudanganywa kampeni meneja wangu alikuwa huyo Songo wakati kampeni meneja wangu ni Fikiri Malenge,” alisema.

Nyerere alisema CCM haikuwa makini katika mambo yake ndiyo maana wakapokea mtu aliyewadanganya, nao wakakubali na kuutangazia umma bila kuhakiki.

Alisema tabia ya kukurupuka kwao inawasababishia kutotimiza ahadi walizozitoa, hasa katika suala la maendeleo, ndiyo maana miradi wanayoifanya inaharibika ama kukumbwa na rushwa pamoja na ufisadi.

Aidha, alisema hofu, kuweweseka na kasi ya wananchi kuhamia CHADEMA vinawapa kiwewe ndio sababu ya kusingizia watu kuhama CHADEMA na kuingia CCM wakidhani watawatisha.

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kuelekea jijini Mbeya, Malenge alikiri kuwa ndiye aliyekuwa kampeni meneja wa Nyerere na ndiye aliyemuwezesha kushinda nafasi ya ubunge akishirikiana na wananchi, hivyo huyo anayejinadi kwa cheo hicho ni muongo.
Malenge alisema kuwa, baada ya kumaliza kampeni alipendekezwa kuwa katibu wa Nyerere na kazi hiyo anaendelea nayo mpaka sasa.

Hivi karibuni, Bulembo alimpokea Songo ambaye alinadiwa kuwa kampeni meneja wa Nyerere, na kachero wa shughuli za usalama na uenezi mkoani Mara kupitia CHADEMA.Chanzo Tanzania Daima


MAMA ATAKA KUJIUA KWA KUNYWA SUMU BAADA YA KUFIWA WATOTO WATATU

comments
Mama mmoja Mkoani Mara, amechukuwa uwamuzi wa kunywa sumu baada ya kugunduwa watoto wake watatu wamefariki dunia, watoto hao walikufa kwa kukosa hewa, baada ya kuacha jiko la mkaa lililokuwa limeinjikwa maharage likiwa linawaka na kwenda kulala.


Mama huyo alichukua uwamuzi huo mgumu na wahatari wa kunywa sumu baada ya kuamka na kugunduwa kuwa watoto wake watatu wamefariki dunia, mama huyo aliwaishwa hospitali na kufanikiwa kutapishwa sumu aliyokunywa.

Watoto hao walikufa kutokana na kukosa hewa katika chumba walichokuwa wamelala ambacho kulikuwa na jiko la mkaa lililokuwa likipika maharage, lna kusababisha
kukosa hewa na kupelekea vifo kwa watoto hao.

Watoto hao watatu waliyofariki ni wanafunzi wa Shule ya
Msingi ya Nyangoto, iliyopo katika Tarafa ya
Ingwe wilayani Tarime Mkoani Mara, Naomi Nyasenso darasa la saba, Magreth Nyasenso darasa la nne na Debora
Nyasenso darasa la kwanza.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime,
Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha, amewashauri wananchi kujenga nyumba na kuweka madirisha makubwa, kwani nyumba hiyo ingekuwa na madirisha
makubwa ya kuingiza hewa, ajali hiyo isingetokea.Chanzo Nifahamishe

HAUKIMIWA KWENDA JELA MIAKA SABA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA

comments
PESA ZA TANZANIA


MAHAKAMA ya wilaya ya Musoma mkoani Mara, imemhukumu kwenda jela miaka 7 mfanyabiashara  Mayai Justine(28) mkazi wa Nyakato Mshikamano kwa kosa la kupatikana na noti bandia.

Akisoma hukumu hiyo  siku ya ijumaa ,mahakamani hapo  , Hakimu mfawidhi mwandamizi wilaya ya Musoma, Richard Maganga baada ya kuridhika na ushahidi  alimhukumu Justine  kutumikia kifungo cha miaka 7.

Mbele ya hakimu, Mwendesha mashtaka wa serikali  Jonas Kaijage amedai kuwa Bw. Mayai Justine ambaye ni mkazi wa Nyakato Mshikamano mjini Musoma  alipatikana na noti bandia za shilingi elfu 50 April 13 mwaka huu na kufikishwa mahakamani Mei 17, 2012.

akitoa hukumu hiyo Hakimu Maganga amesema kupatikana na noti bandia ni kosa la jinai hivyo ametoa hukumu hiyo hili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wanaoweza kufanya kosa kama hilo.


TAFITI ZA KISAYANSI ZINAONYESHA KUWA ULAJI SANA WA NYAMA NYEKUNDU UNASABABISHA UPOFU

comments
ULAJI SANA WA NYAMA NEKUNDU UNASABABISHAUPOFU
Watu wanaopenda sana kula nyama nyekundu kama vile nyama za ng'ombe , mbuzi au 'kitimoto' wana uwezekano mkubwa wa kupata upofu kwenye uzee wao.

 Matokeo ya utafiti wa wanasayansi umegundua kwamba watu wanaopenda kula sana zaidi ya mara kumi kwa wiki nyama za ng'ombe, mbuzi au kondoo na nguruwe wana uwezekano wa asilimia 50 wa kupata upofu kulinganisha na wale wanaokula nyama hizo chini ya mara tano kwa wiki.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa watu wanaopenda sana kula nyama za kuku walionekana kuwa na kinga dhidi ya ugonjwa unaosababisha upofu kutokana na kuharibika kwa retina ya jicho unaojulikana kitaalamu kama Age-related macular degeneration (AMD) ambao husababisha upofu kwa wazee wenye umri zaidi ya miaka 50.

Utafiti huo ulifanywa na chuo kikuu cha Melbourne cha nchini Australia ambapo wanaume na wanawake 5,600 wenye umri wa kwenye miaka ya hamsini na sitini walifanyiwa majaribio kwa miaka 13.

Ingawa ulaji wa nyama nyekundu ulionekana una madhara, watu walioonekana kupenda kula sana nyama ya kuku mara tatu hadi nne kwa wiki walionyesha kuwa na uwezekano mdogo sana wa asilimia 57 kupata upofu kulinganisha na wale waliokuwa wakila nyama za kuku mara moja au mbili kwa wiki.

Ugonjwa wa AMD kawaida huanza kushambulia mtu anapofikisha umri wa miaka 50 ambapo macho huanza kuvuja vimiminika ambavyo huharibu uwezo wa kuona.

Ni mtu mmoja tu kati ya kumi wanaokumbwa na ugonjwa wa AMD hufanikiwa kupata tiba.Chanzo Nifahamishe

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YAWATOA WASIWASI WATANZANIA KUHUSU MFUMO WA DIGITALI

comments
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imewatoa hofu wananchi wote wanaoishi katika maeneo ambayo bado kufikiwa na mfumo mpya wa mawasiliano wa digitali, akisema wataendelea kupata mawasiliano kupitia mfumo wao wa zamani wa analojia.

Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Meneja wa Mawasiliano wa mamlaka hiyo, Innocent Mungi wakati akifafanua kuhusu wasiwasi uliojitokeza kwa wananchi hasa walioko mikoani.
Mungi alisema watazima mtambo wa zamani kule ambako huduma hiyo mpya ya digitali imefika, kwamba kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na mtambo huo, wataendelea kutumia televisheni zao kupitia mfumo wa zamani.

Alibainisha kuwa, hadi sasa ni asilimia 24 sawa na mikoa 11 ya nchi ndiyo itafaidika na mawasiliano hayo ya digitali, ambapo kule kusikokuwa na mawasiliano hayo bado wataendelea kupata mawasiliano kwa kutumia satelaiti, madishi na usambazaji wa nyaya hadi hapo mfumo mpya utakapowafikia.

“Naomba niwatoe hofu wananchi kuwa siyo kweli kwamba ifikapo Desemba 31, serikali itazima mitambo ya analogia nchi nzima, hiyo haiwezekani na wala siyo rahisi kufikisha huduma ya digitali kwa mara moja katika maeneo yote ya nchi,” alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kuwa wasikubali kudanganyika na maneno ya mitaani kuwa ‘televisheni za kichogo’ mara ifikapo mwishoni mwa mwezi huu hazitatumika tena.

Mungi alisema maeneo yote ambayo yamefungwa mtambo huo wa digitali wasitupe televisheni zao kwani zitaendelea kutumika ilimradi wanunue king’amuzi.
Alisema mfumo huo mpya utaleta mapinduzi makubwa katika mawasiliano, zikiwemo faida kama vile huduma zote zilizokuwa zikifanyika katika simu za viganjani.Chanzo Tanzania Daima

MWALIMU AKUTWA AMELALA UCHI KATIKA KIBAO CHA SHULE HUKO LINDI

comments
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.

Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa

Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana  na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema  walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao  kwa muda na badala yake kwenda kukesha  kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.

Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha  mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.

Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule  akiwa uchi wa mnyama.Chanzo Gazeti la Mwananchi

WAKAZI WA INDONESIA WAANZISHA UTAMADUNI WA KUWAFUKUA MAITI NA KUWATEMBEZA MTAANI KABLA YA KUZIKWA TENA

comments
Mmoja ya Maiti ikipambwa kabla ya kufanyiwa Sherehe
Wakazi wa Jimbo la Twaraj Indonesia, wamejiweka utamaduni wa kuwafufua maiti(wafu) na kuwapamba kwa kuwavisha mavazi mapya, kuwachana nywele na kuwatembeza mitaani kabla ya kuwazika tena.
 Dunia imejaa vituko na matukio ya ajabu, hilo limedhihirika hivi karibuni huko nchini Indonesia, katika jimbo la Twaraj, wakazi wa eneo hilo wanatamaduni ya ajabu na ngeni duniani, wakazi hao wanawafufuwa maiti kaburini na kuwavalisha nguo mapya za thamani, kuwachana nywele na kuwapamba kamalive walivyokua hai.

Wakazi hao wanakusanyika na kumfanyia sherehe kubwa maiti kabla ya kuanza msafara wa kumtebeza katika mitaa na kumrejesha kaburini alipokuwa amezikwa, wakazi hao wanamini kwamba watu waliyokufa wanahaki ya kuendelea kuishi na kujumuika nao.

katika kufanikisha zoezi hilo la kihistoria ambalo wanaimani kwa lazima kufanya ili kuonesha hishima kwa maiti na kulinda mapenzi ya kweli kwa mtu aliyekufa, kabla ya kumzika maiti anavishwa kitambaa maalum ili kuzuia mwili wa marehemu kuoza.Chanzo Nifahamishe

MFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI AMNYWESHA MKOJO BOSI WAKE KWA KUMCHELEWESHEA MSHAHARA

comments
MFANYAKAZI za ndani ‘hausigeli’ amehukumiwa kifungo cha miezi miwili jela na viboko, kwa kosa la kumnywesha mkojo bosi wake kutokana na hasira ya kutolipwa mshahara wake kwa wakati.

Rita Chakwesha mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliajiriwa katika nyumba iliyopo kwenye Barabara ya Avenue mjini Harare, kwa makusudi alimnywesha mwajiri wake Sharlotte Chivavarirwa maji yaliyokuwa na mkojo ndani yake.

Chakwesha alionekana mbele ya Hakimu Barbra Masinire huko Harare, akihukumiwa kwa makosa hayo, huku akijitetea kuwa alikuwa akifanya hivyo kutokana na kutopewa ujira wake kwa miezi miwili.

Mshauri wa Jimbo la Francesca Mukumbiri aliiambia mahakama kuwa Novemba 5 majira ya saa 11 jioni, Chivavarirwa alirejea nyumbani akitokea kazini, na mara baada ya kufika alimwomba msichana wake wa kazi Chakwesha ampe maji kutoka katika jokofu.

Chakwesha alienda na kumiminia maji ambayo tayari alikuwa ameyatia mkojo na kumpa bosi wake kwamba ayafurahie kwani ni maji yaliyokuwa na ladha nzuri.

Mama huyo mwenye nyumba baada ya kufungua jokofu aliona glasi yenye kitu chenye rangi ya manjano na harufu mbaya, hivyo akahisi kuwa huenda ni mkojo.

Hata hivyo, Chakwesha hakuishia hapo, alijikuta akitoa siri kwa rafiki wa karibu na Chivavarirwa, ambaye hakutaka kuitunza siri ile.

Rafiki huyo alikwenda kumweleza hali halisi Chivavarirwa ambaye aliamua kulipeleka suala hilo chini ya sheria na hivyo Chakwesha alikamatwa.

Kabla ya kuburutwa mahakamani, Chakwesha alikiri kutenda kitendo hicho cha ajabu na kwamba hali hiyo ilitokana na mwajiri wake kutomlipa ujira wake “Ndanga ndabatwa nemweya wehutsinye,” Chakwesha aliiambia mahakama.Chanzo Gazeti la Mwananchi

MWANAMKE AKERWA KUPEWA TARAKA KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK

comments
Emma na Nail Brady wakati wa Harusi Yao
Mwanamke mmoja nchini Uingereza alipigwa na butwaa baada ya kugundua kwamba ndoa yake ya miaka sita imefikia tamati baada ya kugundua kwamba mumewe amemuachia talaka kwenye mtandao wa Facebook.


Emma Brady, 39, alisema kwamba aligundua kwamba ameachika baada ya kupigiwa simu na rafiki yake baada ya rafiki yake huyo kuona talaka yake kwenye mtandao wa Facebook.

Ujumbe uliorushwa kwenye mtandao huo ulisomeka "Neil Brady ameamua kuvunja ndoa yake na Emma Brady."

Bi Brady aliielezea aibu aliyoisikia na hasira kutokana na talaka hiyo iliyowekwa kwenye mtandao na kusomwa na watu kadhaa. Emma aliiambia mahakama ya Blackburn ambayo mume wake mwenye umri wa miaka 39 mtaalamu wa IT alikutwa na hatia ya kumshambulia.

"Nilijisikia vibaya sana kutokana na tukio hili. Watu wote ambao ninawasiliana nao kwenye mtandao ni watu ambao nimejuana nao kwa miaka mingi, nilijihisi kuaibishwa sana kwa jambo hili kuwekwa wazi katika mtandao" alisema.

"Kama angekuwa amenijulisha kwamba anataka tuachane ningemkubalia kwasababu nisingependa awe hana furaha".

Emma Brady, meneja wa makongamano na mama wa mtoto mmoja alisema kwamba alikuwa hajui kama kuna ujumbe huo wa mumewe kwenye mtandao mpaka pale alipopigiwa simu na rafiki yake aliyepo Denmark kujuliwa hali.

"Tulikuwa tukiishi kama wanandoa wengine kukiwa kuna wakati malumbano ya hapa na pale na wakati wa furaha . Kwa jinsi nilivyokuwa nafahamu tulikuwa tunaishi vizuri tu" aliiambia mahakama.

"Nilipata mshtuko baada ya simu hiyo na kutaka kumpigia simu Neil lakini marafiki zangu walinishauri nionane naye uso kwa uso".

"Nilipofika nyumbani nilimuuliza Neil kama ana chochote cha kunieleza lakini alijifanya kama hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea".

Mwishoni Neil alishindwa kujizuia hasira zake na kumtoa mkewe kwa nguvu nje ya nyumba hiyo akiwa amevaa gauni la kulalia tu na kumjeruhi mkono wake kabla ya kumfungia uwani mwa nyumba hiyo.

Neil alimshutumu Emma kwamba alikuwa akitoka nje ya ndoa na mwanaume mwingine, huku wakati huohuo akijaribu kuchukua simu ya Emma kwa nguvu kuangalia meseji katika simu yake.

Neil alikutwa na hatia ya kumshambulia Emma na kupigwa faini ya paundi 580 na kutakiwa kulipa fidia ya paundi 100 na paundi 75 za gharama alizosababisha.

Wanandoa hao hivi sasa wanaishi sehemu tofauti wakijianda kwenda mahakamani kuivunja ndoa yao kisheria.Chanzo Nifahamishe

ZANZIBAR HEROES YAFUTWA KWA UTOVU WA NIDHAMU KWA KUGAWANA FEDHA BILA UONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA ZANZIBAR

comments
Kikosi cha Timu ya Zanzibar Heroes
Kikosi cha timu ya Zanzibar Heroes kimefutwa kwa
utovun wa nidhamu, baada ya kushika nafasi ya tatu kikosi hicho katika
michuano ya CECAFA, wamegawana fedha bila ya uongozi wa chama cha mpira Zanzibar kufahamu.
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimechukua uwamuzi wa kuivunja rasmi timu ya taifa,
Zanzibar Heroes kufuatia kitendo utovu wa nidhamu kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo,kuamuwa kugawana fedha walizopata baada ya kushika
nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki
na Kati, CECAFA Tusker Challenge yaliyomalizika hivi karibuni mjini
Kampala, Uganda.

Timu ya Zanzibar heroes ilizawadiwa kiasi cha dola za Kimarekani
10,000 baada ya kuifunga timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars kwa
penalti 6-5, baada ya kumalizika mchezo kwa sare ya 1-1.

Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai
kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao kila wanaposhiriki katika
mashindano ya kimataifa, kutokana na kitendo hicho Chama cha Soka
Zanzibar (ZFA), kimewafungia wachezaji 16, kwa muda usiyojulikana
kucheza soka popote duniani.
ZFA.

Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, akielezea tukio hilo amesema
haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao,
akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano
kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa
ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu na mara zote walipewa
stahili zao.Chanzo Nifahamishe

 

TETESI ZIMEENEA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUWA MIKE TYSON ADAIWA KUBADILISHA JINSIA

comments
MIKE TYSON

BINGWA wa zamani wa ndondi uzito wa juu, Mike Tyson anadaiwa kubadilisha jinsia kutoka kuwa hali ya kiume na kuwa kike.

Habari za kufanyiwa upasuaji huyo kwenye hospitali moja mjini, Beverley Hills, Marekani ziliteka mitandao kadhaa ya kijamii, huku pia gazeti la The Standard likiwa na habari hiyo.
Hata hivyo, habari hizo hazijathibitishwa ramsi ingawa mpaka jana jioni mitandano mingi ya kijamii ilikuwa na taarifa hizo.

Bingwa huyo wa zamani aliyejitaja kama Ć«Mwanaume mbaya dunianiĆ­, mzaliwa wa Brooklyn, aliwaambia waandishi wa habari kuwa siku kwanza atakayopata hedhi (kuona siku zake) ndiyo itakuwa kamilisho la ndoto yake.

Lakipi pia katika kuhakikisha anakamilisha dhamira yake ya kuwa mwanamke, amesema kuanzia muda huo jina lake ramsi sasa litakuwa Michelle.

Baadhi ya watu wanaweza kudhani mimi ni mtu wa ajabu kwa sababu sasa ni mwanamke," alisema bingwa huyo wa zamani wa ndondi aliyewahu kuhukumiwa kwa shitaka la kubaka.
Upasuaji wa kubadilisha jinsia ya Tyson ulichukua takribani masaa 16, akibadilishwa sura, rangi na mambo mengine ya kumfanya avutie kama mwanamke.

Pamoja na ubabe wangu ulionifanya kuwa mpiganaji mzuri, sikuwahi kupoteza hali yangu ya uanamke na nilijua ipo siku moja matiti yataota na pia nitakuwa na sehemu za siri za mwanamke.
Tyson, maarufu kama 'Iron Mike au Iron Maiden', aliyewahi kumng'ata meno bondia, Evander Holyfield walipodundana mwaka 1996, alipandikizwa homoni za kike zitakazomfanya kuwa na tabia za jinsia hiyo.
Tyson, akiwa amevalia wigi, suruali aina jeans yenye nyeusi na fulana ya rangi ya Bluu na kuonekana mwenye furaha, alisema kubadilishwa kwake viungo na kuwekwa vya kike, kunathibitisha mwisho wa tabia yake mbaya.

Pamoja na watangazaji wa ndondi kushangazwa na hatua hiyo ya Tyson, lakini wengi wamekubali kwamba kuna mabadiliko ya kitabia yameonekana. "Amabadilisha kimavazi, mwonekano na kizuri zaidi amekuwa mpole," taarifa zilidai.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali za uzushi zikiwahusu watu maarufu, ambapo katika ya mwaka huu msanii Eddie Murphie alidaiwa kufa katika ajali ya boti ya kuteleza kwenye barafu.
Msanii mwingine aliyehushishwa na uzushi huo ni Will Smith ambaye naye alikumbwa na kadhia ya kudaia kufa. Wote wako hai mpaka sasa.Chanzo gazeti la Mwananchi