MWANAMKE AKERWA KUPEWA TARAKA KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK

Emma na Nail Brady wakati wa Harusi Yao
Mwanamke mmoja nchini Uingereza alipigwa na butwaa baada ya kugundua kwamba ndoa yake ya miaka sita imefikia tamati baada ya kugundua kwamba mumewe amemuachia talaka kwenye mtandao wa Facebook.


Emma Brady, 39, alisema kwamba aligundua kwamba ameachika baada ya kupigiwa simu na rafiki yake baada ya rafiki yake huyo kuona talaka yake kwenye mtandao wa Facebook.

Ujumbe uliorushwa kwenye mtandao huo ulisomeka "Neil Brady ameamua kuvunja ndoa yake na Emma Brady."

Bi Brady aliielezea aibu aliyoisikia na hasira kutokana na talaka hiyo iliyowekwa kwenye mtandao na kusomwa na watu kadhaa. Emma aliiambia mahakama ya Blackburn ambayo mume wake mwenye umri wa miaka 39 mtaalamu wa IT alikutwa na hatia ya kumshambulia.

"Nilijisikia vibaya sana kutokana na tukio hili. Watu wote ambao ninawasiliana nao kwenye mtandao ni watu ambao nimejuana nao kwa miaka mingi, nilijihisi kuaibishwa sana kwa jambo hili kuwekwa wazi katika mtandao" alisema.

"Kama angekuwa amenijulisha kwamba anataka tuachane ningemkubalia kwasababu nisingependa awe hana furaha".

Emma Brady, meneja wa makongamano na mama wa mtoto mmoja alisema kwamba alikuwa hajui kama kuna ujumbe huo wa mumewe kwenye mtandao mpaka pale alipopigiwa simu na rafiki yake aliyepo Denmark kujuliwa hali.

"Tulikuwa tukiishi kama wanandoa wengine kukiwa kuna wakati malumbano ya hapa na pale na wakati wa furaha . Kwa jinsi nilivyokuwa nafahamu tulikuwa tunaishi vizuri tu" aliiambia mahakama.

"Nilipata mshtuko baada ya simu hiyo na kutaka kumpigia simu Neil lakini marafiki zangu walinishauri nionane naye uso kwa uso".

"Nilipofika nyumbani nilimuuliza Neil kama ana chochote cha kunieleza lakini alijifanya kama hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea".

Mwishoni Neil alishindwa kujizuia hasira zake na kumtoa mkewe kwa nguvu nje ya nyumba hiyo akiwa amevaa gauni la kulalia tu na kumjeruhi mkono wake kabla ya kumfungia uwani mwa nyumba hiyo.

Neil alimshutumu Emma kwamba alikuwa akitoka nje ya ndoa na mwanaume mwingine, huku wakati huohuo akijaribu kuchukua simu ya Emma kwa nguvu kuangalia meseji katika simu yake.

Neil alikutwa na hatia ya kumshambulia Emma na kupigwa faini ya paundi 580 na kutakiwa kulipa fidia ya paundi 100 na paundi 75 za gharama alizosababisha.

Wanandoa hao hivi sasa wanaishi sehemu tofauti wakijianda kwenda mahakamani kuivunja ndoa yao kisheria.Chanzo Nifahamishe

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE