HOSPITALI YA MKOA WA MARA INAKABILIWA NA UPUNGUFU WA BAADHI YA DAWA
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara Iragi Ngerageza |
Akiongea na chibasa blogspot mganga mfawidhi w badoa hospitali hiyo Iragi Ngerageza amesema kuwa bohari ya dawa imekuwa ikiwapa dawa ambazo hazitoshelezi mahitaji ya hospitali hiyo.
Amesema kuwa hivi karibuni hospitali hiyo imenunua dawa kwenye bohari ya dawa zenye thamani ya shilingi 41,190,100 lakini bado kuna mahitaji ya baadhi ya dawa hali inayosababisha wananchi kwenda kununua madawa kwenye maduka ya mitaani.
Katika kukabiliana na tatizo hilo tayari uongozi wa hospitali kupitia kamati yake inafanya jitahada ya kununua dawa ambazo hawakuzipata kutoka bohari ya dawa (msd) kwenda kununua dawa hizo kwenye maduka ya watu binafsi ambayo yameteuliwa na serikali.
“Wananchi wanatakiwa kuelewa kuwa tunaupungufu wa baadhi ya dawa lakini tunafanya jitahada za kununua dawa hizo ili kuwawezesha wananchi kupata dawa hizo” alisema
Ili kukabiliana na changamoto hiyo ameiomba serikali kuiwezesha bohari ya dawa kutoa dawa kulingana na mahitaji husika ili kuboresha huduma ya afya kwa jamii hususani wale wanaokwenda kutibiwa katika hospitali hiyo.
Comments
Post a Comment