Posts

KABURI LA MTOTO ALIYEFARIKI MIAKA MITATU ILIYOPITA LAFUKULIWA BAADA YA KUONEKANA YUKO HAI

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kaburi ambalo alizikwa mtoto Shabani Maulidi (15), ambaye anadaiwa kufariki dunia miaka mitatu iliyopita na kuonekana akiwa hai hivi karibuni, jana lilifukuliwa na viungo vya mwili wake kukutwa ndani. Kazi hiyo iliyofanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Mtafiti wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Lucas Ndungulu, ilizua taharuki kwa umati wa watu waliokuwa eneo hilo, baada ya nyumba ya jirani lilipo kaburi hilo, Masanja Marwa, kubomoka ghafla wakati ufukuaji huo ukiendelea, huku mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja naye akianguka na kuzirai. Kwa sasa mtoto huyo ambaye alionekana hai, amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa uangalizi wa kitaalamu. Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Ndungulu alisema kuwa wameamua kufukua kaburi hilo ili kupata sehemu ya viungo vya mwili kwa ajili ya vipimo. “Lengo la kufukua kaburi hili ni kutaka tupate kiungo chochote cha ...

WATAKAO FELI MTIHANI WA KIDATO CHA PILI KURUDIA DARASA

Image
Wanafunzi Wakati wanafunzi wa kidato cha pili wakitarajia kufanya mtihani wa taifa wiki ijayo, Serikali imesema watakao feli watarudia darasa hilo. Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi profesa Sifuni Mchome alipokua akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam. Alisema jumla ya wanafunzi 531, 457 wa kidato cha pili wanatarajia kufanya mtihani huo nchi nzima. “ watakao feli watarudia darasa hilo na watakao feli mara ya pili serikali itaangalia uwezekano wa kuwapeleka shule za ufundi au kuendelea na shule kama wanafunzi wa kujitegemea” alisema Profesa sifuni. Alisema mtihani huo utaanza October 7 hadi 21 mwaka huu katika vituo takribani 4,437 vilivyosajiliwa kwa ajili ya kufanyia mitihani nchi nzima na wanafunzi waliojiandikisha kufanya mitihani hiyo wasichana ni 270,734 sawa na asilimia 50.1 na wavulana ni 260,723 sawa na asilimia 49.1 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 3.1 ikilinganishwa na watahiniwa wa mwaka jana ...

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEMFUKUZA KAZI ASKARI ALIYEINGIA UKUMBI WA DISCO AKIWA NA BUNDUKI

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu na majambazi, maarufu kama Kimbunga, Simon Sirro, amesema kuwa wamemtimua askari wao aliyeingia ukumbi wa disko mjini Bukoba akiwa na bunduki kwa ajili ya kulipa kisasi. Sirro alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jana wakati akielezea mafanikio waliyoyapata katika operesheni hiyo kwa kuwakamata watuhumiwa 88 wanaojihusisha na ujambazi na biashara ya silaha. Alimtaja askari huyo kuwa ni mwenye namba H 85, PC Alphonce, aliyekuwa ametokea mkoani Mara kwa ajili ya kushiriki operesheni hiyo mkoani Kagera. Alisema kuwa PC Alphonce alikorofishana na baadhi ya watu ndani ya ukumbi wa disko, hivyo akatoka nje kufuata bunduki, kisha akarudi nayo kwa ajili ya kuwadhuru ‘wabaya’ wake, lakini askari wenzake waliokuwamo ndani walifanikiwa kumzuia kabla ya kutimiza azima yake. Kuhusu kukamatwa kwa Mkurugenzi wa redio ya kijamii iliyoko wilayani Karagwe (FADECCO) na kuwekwa ndani siku mbili, kis...

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MARA KUBORESHA MAHUSIANO

Wito umetolewa kwa wanasiasa na wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoani Mara kuacha Siasa za makundi ndani ya chama ili kukimalisha na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) Mkoani Mara Bwana Christopher Mwita Sanya, alipokua akijibu maswali mbalimbali toka kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mara katika ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa nyasho mjini Musoma. Sanya amesema siasa za makundi hazitakiwi kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla na tayari chama hicho kimeanza vikao vyenye lengo la kuondoa makundi na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Amesema chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kuwakumbusha madiwani na wabunge wa chama hicho kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ili kurejesha imani kwa wananchi kuwa ahadi wanazotoa katika chaguzi mbalimbali wanazitekeleza. Mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi mkoani mara leo amefanya kikao hicho na waandishi wa habari kwa len...

MUDA WA KUBADILISHA LESENI SASA MWISHO APRIL 31

Matatizo ya kukatika kwa umeme ni miongoni mwa sababu zilizosababisha polisi nchini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kuongeza muda wa utoaji wa leseni mpya hadi Aprili 31 mwaka huu badala ya Machi 31 iliyopangwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema wamelazimika kuongeza siku baada ya kubaini kuwapo kwa mambo kadhaa yaliyokwaza baadhi ya madereva kubadilisha leseni zao kama inavyotakiwa. “Tumebaini madereva hao walishindwa kubadili leseni zao kutokana na kukosekana kwa mtandao ambao ndiyo unawezesha mawasiliano ya kielektroniki kati ya TRA na trafiki, ingawa pia siku za kazi ziliingiliana na Sikukuu ya Pasaka’’ alisema. Alisema baadhi ya madereva wengine nao  hawajamaliza mafunzo yao ya PSV katika Vyuo vya NIT na Veta huku wengine wakichelewa kupewa vyeti vyao licha ya kumaliza mafunzo hayo,”alisema Mpinga. Alisema kutokana na sababu hizo wameamua kuongeza muda ikiwa n...

SERIKALI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WATAKAOTUMIA VIBAYA SIMU NA MITANDAO YA KIJAMII

SERIKALI imesema itachukua hatua kali za kisheria kwa atakayebainika kutumia vibaya simu za mkononi, na mitandao ya kijamii kuleta uchochezi au kwenda kinyume na maadili ya nchi. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa alipozungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka kukomesha vitendo hivyo. “Hatua hizo zitachukuliwa dhidi ya kampuni au mtu yeyote atakayetoa kashfa na kuitukana serikali, viongozi wa serikali, dini, siasa na watu binafsi,” alisema na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinakiuka sheria za nchi. Alisema hatua hizo pia zitawakumba watu wote wanaojihusisha na uonyeshaji wa picha za ngono kwenye mitandao, unyanyasaji wa watoto na ukiukaji wa maadili na kutoa taarifa zenye lengo la kuvunja utulivu na amani. “Matumizi mabaya ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) kama simu za mikononi, barua pepe, na mitan...

BUSH PARTY KUFANYIKA SIKU YA PASAKA KATIKA UFUKWE WA BWALO LA POLISI MWISENGE

Image
Hawa ndio The The Track Masters DJs na Hii ilikua ni siku ya mwaka mpya tulipoangusha bonge la burudani pale bwalo la polisi mwisenge na sasa The track Masters Djs wakishirikiana na Mimi Entertainments & Promotions  tumekuandalia BUSH PARTY ni katika ufukwe wa bwalo la polisi mwisenge kutakua na burudani mbalimbali za toka kwa wasanii wa asili na wasanii mbalimbali wa shows za sebene. Kama kawaida Bonge la Disco kutoka kwa The Track Masters Djs hapa namzungumzia Dj Lima pamoja na Dj Chibarland tutafanya yetu na ww karibu ufanye yako. Burudani itaanza saa nane kamili mchana mpaka choka mwenyewe KINGILIO- Watoto 1000/= na WAKUBWA 2000/= Nyote mnakaribishwa. Imedhaminiwa na AURIC AIR, COCA COLA na POLISI MESS Bwalo la Polisi mwisenge ndio Wadhamini wakuu wa show yetu ya BUSH PARTY siku ya pasaka kumbuka vinywaji vinapatikana kwa bei poa kabisa ya 1500 kwa vinywaji vya TBL karibuni sana kwa burudani na huduma ya vinywaji karibu na bureeeeee ukikosa hii shauri yako Wadhami...