WATAKAO FELI MTIHANI WA KIDATO CHA PILI KURUDIA DARASA
Wanafunzi |
Wakati wanafunzi wa kidato cha pili wakitarajia kufanya
mtihani wa taifa wiki ijayo, Serikali imesema watakao feli watarudia darasa
hilo.
Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wizara ya elimu na
mafunzo ya ufundi profesa Sifuni Mchome alipokua akizungumza na waandishi wa
habari jijini dar es salaam. Alisema jumla ya wanafunzi 531, 457 wa kidato cha
pili wanatarajia kufanya mtihani huo nchi nzima.
“ watakao feli watarudia darasa hilo na watakao feli mara ya
pili serikali itaangalia uwezekano wa kuwapeleka shule za ufundi au kuendelea
na shule kama wanafunzi wa kujitegemea” alisema Profesa sifuni.
Alisema mtihani huo utaanza October 7 hadi 21 mwaka huu
katika vituo takribani 4,437 vilivyosajiliwa kwa ajili ya kufanyia mitihani
nchi nzima na wanafunzi waliojiandikisha kufanya mitihani hiyo wasichana ni
270,734 sawa na asilimia 50.1 na wavulana ni 260,723 sawa na asilimia 49.1
ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 3.1 ikilinganishwa na watahiniwa wa mwaka
jana ambao walikua 4,297.
Aidha alisema kwa upande wa makundi maalum yenye mahitaji
maalumu wenye uoni hafifu ni 89 na wasiona ni 93.
Comments
Post a Comment