KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?
Kati ya Kuku na Yai Kipi Kilianza? Mjadala wa miaka mingi kuhusiana na kipi kilitokea mwanzo kuku au yai? umepata jibu baada ya wanasayansi kuthibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo awali kabla ya yai. Mjadala wa miaka nenda rudi kuwa kuku na yai kipi kilitangulia duniani umepatiwa jibu na wanasayansi wa nchini Uingereza ambao wamethibitisha kuwa kuku ndiye aliyekuwepo mwanzo kabla ya yai. Kwa kuangalia jinsi ganda la yai lilivyotokea, wanasayansi wa nchini Uingereza wanaamini wamepata jibu la mjadala huo. Watafiti katika vyuo vikuu vya Sheffield na Warwick nchini Uingereza wamegundua kuwa protini inayoitwa ovocleidin (OC-17) ni muhimu sana katika kutengenezwa kwa gamba la yai. Lakini protini hiyo hupatikana toka kwenye ovari ya kuku mwenye ujauzito. Kwa maana hiyo yai lisingekuwepo kama kusingekuwa na protini ambayo inatoka kwa kuku mjamzito. Watafiti hao waliongeza kuwa protini ya OC-17 husababisha calcium carbonate kwenye mwili wa kuku ibadilike kuwa calcite crys
Comments
Post a Comment