MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MARA KUBORESHA MAHUSIANO



Wito umetolewa kwa wanasiasa na wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoani Mara kuacha Siasa za makundi ndani ya chama ili kukimalisha na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) Mkoani Mara Bwana Christopher Mwita Sanya, alipokua akijibu maswali mbalimbali toka kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mara katika ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa nyasho mjini Musoma.

Sanya amesema siasa za makundi hazitakiwi kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla na tayari chama hicho kimeanza vikao vyenye lengo la kuondoa makundi na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho.

Amesema chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kuwakumbusha madiwani na wabunge wa chama hicho kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ili kurejesha imani kwa wananchi kuwa ahadi wanazotoa katika chaguzi mbalimbali wanazitekeleza.

Mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi mkoani mara leo amefanya kikao hicho na waandishi wa habari kwa lengo la kuboresha mahusiano kati ya waandishi wa habari na chama hicho.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE