WANAFUNZI WA MARA SEKONDARI WAANDAMANA WAKIDAI MATIBABU BORA NA CHAKULA BORA
WANAFUNZI WA MARA SEKONDARI WAKIWA KATIKA MAANDAMANO |
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mara iliyopo
Manispaa ya Musoma mkoani Mara leo wameandamana kuelekea ofisi za mkoa kile wanachodai kuwa katika shule hiyo hakuna
utaratibu bora wa matibabu na kubadilishiwa ratiba ya Chakula.
Wakiongea mbele ya Afisa Elimu Mkoa wa Mara Bw Hamis Lisu katika
viwanja vya Posta Manispaa ya Musoma, Baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa
kubadilika kwa ratiba ya chakula na kutokuwepo kwa huduma bora za matibabu ndio
hali iliyopelekea wao kuandamana ili kufikisha kilio chao katika ngazi ya mkoa.
Wamesema kuwa walipokuwa kidato cha tano ratiba ya kula wali,nyama
pamoja na mboga za Majani ilikuwa ni mara mbili kwa wiki lakini tangu January
Mwaka huu walielezwa kubadilika kwa ratiba ya chakula kutokana na kugoma kwa
mzabuni na hivyo kula wali na nyama mara moja kw wiki huku mboga za
majani hazipatikani kabisa kama wanavyobainisha Alex Mirumbe pamoja na Emmanuel
William.
Akiongea mara baada ya kuwasikiliza wanafunzi hao,Afisa elimu Mkoa
wa Mara Bw Hamis Lisu aliwaahidi wananfunzi hao kukutana na uongozi wa wilaya
na kisha kwenda shuleni hapo ili kutatua madai ya wanafunzi hao.
Mwisho
Comments
Post a Comment