Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma



Wimbi la mauaji limeendelea kushika kasi katika mkoa wa Mara ambapo mnamo tarehe 19/2/2013 katika mtaa wa kawawa kata ya mwigobero manispaa ya Musoma Sabina Dominico aliuwawa kwa kunyongwa kwa kutumia pazia.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalom Mwakyoma kwa waandishi wa habari binti huyo mwenye miaka 21 alitendewa unyama huo majira ya saa kumi na moja jioni nyumbani kwa magori chacha mfanyabiashara ya mafuta.

Taarifa hiyo imeleza kuwa mwili wa marehemu ulikutwa umefungwa mikono na miguu na kisha kamba iliyomnyonga shingoni ni kipande cha pazia alichochanachana.
Kabla ya kutekeleza mauaji hayo,Mtuhumiwa huyo ambaye nae alijinyonga kwa kutumia kamba ya manira kwa kujitundika kwenye chuma kinachobeba tanki la maji aina ya simtank na kabla ya kujinyonga alimjeruhi tumboni mke wa mfanyabiashara huyo  Mugesi Magori Chacha  ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa mara kwa matibabu.

Chanzo cha tukio hili bado hakijafahamika na uchunguzi wa kina unafanyika ili kuepuka maafa zaidi.


 NA HUKO DAR ES SALAAM


MHITIMU wa kidato cha nne jijini Dar es Salaam, Barnaba Venant (18), amejinyonga baada ya kutoridhishwa na matokeo ya mtihani wake, yaliyotangazwa juzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Englibert Kiyondo, alisema tukio hilo la kusikitisha lilitokea juzi, majira ya saa nne asubuhi katika eneo la Nzasa, Mbagala ambapo kijana huyo alijinyonga kwa kutumia kamba ya manila, aliyotundika kwenye dari ndani ya stoo ya nyumba yao.

Kiyondo alisema Venant alimaliza kidato cha nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari Debrabant, Mbagala, huku akielezea kuwa sababu ya kujinyonga kwake ni kutoridhishwa na matokeo ya mtihani wake ambapo alipata daraja la nne la pointi 27, kinyume na matarajio yake.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke wakati upelelezi wa tukio hilo unaendelea.

Matokeo kidato cha nne mwaka huu, yamekuwa gumzo kutokana na kiwango cha ufaulu kushuka kwa kasi ya kutisha.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, jumla ya watahiniwa 240,903, sawa na asilimia 60 ya watahiniwa wote, wamepata ziro ambapo kati yao wasichana ni 120,239 na wavulana 120,664.

Wakati huohuo, watu wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti, likiwemo la mkazi wa Kisensera Bunju B, Miraji Sewia (30) kukanyagwa na gari baada ya kulidandia na kudondoka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi katika barabara ya Bunju eneo la Kisensera ambapo gari aina ya Fuso yenye namba za usajili T 614 AQX iliyokuwa ikiendeshwa na Freddy Ndenasi (45) ilimkanyaga Sewia na kufariki papohapo.

Katika hatua nyingine, Kamanda Kenyela alisema mkazi wa Mikocheni alijefahamika kwa jina moja la Mzee Selemani, amefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema chanzo cha kifo hicho hakijafahamika na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi : chanzo Gazeti la Tanzania Daima


Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE