ZANZIBAR HEROES YAFUTWA KWA UTOVU WA NIDHAMU KWA KUGAWANA FEDHA BILA UONGOZI WA CHAMA CHA MPIRA ZANZIBAR
Kikosi cha Timu ya Zanzibar Heroes |
Kikosi cha timu ya Zanzibar Heroes kimefutwa kwa utovun wa nidhamu, baada ya kushika nafasi ya tatu kikosi hicho katika michuano ya CECAFA, wamegawana fedha bila ya uongozi wa chama cha mpira Zanzibar kufahamu. |
||
Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kimechukua uwamuzi wa kuivunja rasmi timu ya taifa, Zanzibar Heroes kufuatia kitendo utovu wa nidhamu kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo,kuamuwa kugawana fedha walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge yaliyomalizika hivi karibuni mjini Kampala, Uganda. Timu ya Zanzibar heroes ilizawadiwa kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 baada ya kuifunga timu ya taifa ya Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, baada ya kumalizika mchezo kwa sare ya 1-1. Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao kila wanaposhiriki katika mashindano ya kimataifa, kutokana na kitendo hicho Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), kimewafungia wachezaji 16, kwa muda usiyojulikana kucheza soka popote duniani. ZFA. Katibu Mkuu wa ZFA Taifa, Kassim Haji Salum, akielezea tukio hilo amesema haijawahi kutokea wachezaji wa timu hiyo kudhulumiwa haki yao, akikumbushia fedha za zawadi walizopata mwaka 1995 katika mashindano kama haya yaliyofanyika nchini Uganda na Zanzibar ikafanikiwa kutwaa ubingwa na mwaka 2009 waliposhika nafasi ya tatu na mara zote walipewa stahili zao.Chanzo Nifahamishe |
||
|
Comments
Post a Comment