TELEVISHENI ZOTE ZENYE LESENI KITAIFA SASA KUANZA KUONEKANA KWENYE KING'AMUZI


Mamlaka  ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa televisheni za ndani zitakazoingizwa kwenye ving’amuzi ni zile zenye leseni ya kitaifa tu.

TCRA imesema kwamba zile ambazo leseni zake ni za maeneo kama vile wilaya, mkoa na  kijiji, utaratibu wa kuingizwa kwenye ving’amuzi utaanza Januari mwakani.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni njia ya kuelekea kwenye mfumo wa teknolojia ya dijitali ambapo Tanzania itaingia rasmi Januari mwakani na kwamba mitambo yote ya analogia itazimwa Desemba 31, mwaka huu saa sita usiku.

Akizungumza jana kwenye uzinduzi wa tangazo na wimbo wa kuhamasisha uhamaji wa teknolojia ya utangazaji kutoka analogia kwenda dijitali, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA , Habi Gunze alisema, utaratibu wa kuhamia dijitali ni wa lazima na si wa hiari.

Alisema televisheni ambazo bado kuingizwa kwenye ving’amuzi kama zile za dini na nyinginezo, zitaingizwa ifikapo Januari mwakani.

Gunze alisema televisheni hizo nyingi leseni zake ni za maeneo, wilaya au mkoa hivyo mchakato wake uko katika hatua ya mwisho kuingizwa.

Televisheni zilizoingizwa kwenye ving’amuzi ni za TBC, ITV, Star, Channel 10 na Clauds.

Aliwataka wananchi kufanya maandalizi haraka ya kuingia kwenye dijitali kwa kununua ving’amuzi na wasidanganywe na watu au mafundi kuwa televisheni zao ni mbovu au hazifai kutumika kwenye mfumo huo.

Aliwataka kununua ving’amuzi kwa mawakala wa kampuni zilizopewa leseni na TCRA na kuwahimiza kuchukua risiti na gerentii ili kinapokuwa na matatizo, wawasiliane haraka na wakala husika.

Kampuni zilizopewa idhini ya kuingiza ving’amuzi ni Star Media, Agape Associates Ltd na Basic Transmitions Tanzania Ltd.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa tangazo hilo, msanii marufu nchini, Mrisho Mpoto ambaye ndiye aliyeimba wimbo wa kuhamasisha kutoka analogia kwenda dijitali na  wengine akiwemo Banana Zolo, alisema ni shuhuda mzuri kwa baadhi ya wananchi wanavyodanganywa kuhusu televisheni.

Alisema ameshuhudia wafanyabiashara wakienda vijijini kuwarubuni wananchi kuwa televisheni zao hazitafanya kazi baada ya Desemba 31.

“Sasa wengi wanaona ni bora kupata nusu hasara, hivyo huamua kuziuza televishenmi zao kwa bei nafuu sana,” alisema na kusisitiza kuwa elimu inahitajika kwa wananchi juu ya mfumo huo mpya.Chanzo ipp media

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE