NGARIBA HUKO MUGUMU WILAYANI SERENGETI WAMESEMA WATAACHA SHUGHULI HIYO PINDI WAZAZI WATAKAPO ACHA KUWAPELEKA WATOTO KWAO KWA AJILI YA KUKEKETWA

BAADHI ya wanawake wanaoendesha vitendo vya ukeketaji watoto wa kike, maarufu kwa jina la Ngariba, wilayani Serengeti, Mara, wamesema hawawezi kuacha kazi hiyo hadi pale wazazi wenyewe watakapoacha kuwapelekea watoto wao kwa ajili ya kuwakeketa.

Akiwawakilisha wenzake juzi, mmoja wa mangariba hao, Agnes Thomas, ambaye ameshiriki kikao cha kupiga vita ukeketaji, kilichoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la Mara Inter African Commitee, alisema ni vigumu kuacha kazi hiyo, kwani bado wazazi wengi, wana mwamko wa kuwapelekea watoto wao, ili wakeketwe kwa lengo la kutimiza mila zao.

Agnes alisema pamoja na kazi hiyo kuwapatia kipato, lakini ngariba wanaweza kuiacha pale tu wazazi na walezi, watakapobadilika na kuacha tabia ya kuwapelekea watoto.
Aidha, wazee wa kimila walioshiriki kwenye kikao hicho, walishauri ili kukomesha ukeketaji; elimu inapaswa kutolewa, ili jamii ifahamu madhara yake.

Aidha, katika kikao hicho wazee wa kimila pia walipendekeza itafutwe njia mbadala ya kukeketa watoto wa kike, ili waweze kutimiza mila zao.

Moja ya njia waliyopendekeza ni kimwingiza msichana katika chumba kinachotumika kukeketea na kisha kuwamwagia unga na kumpaka usoni bila ya kumkeketa.Chanzo Ahmed Makongo

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS