LEMA ATEMA CHECHE KWA WAKAZI WA BUNDA KATIKA MKUTANO WA HADHARA

GODBLESS LEMA AKIWAHUTUBIA WAKAZI WA MJINI BUNDA


CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kimemvaa mbunge wa jimbo la Bunda Bw. Stephen Wasira jimboni kwake na kuwataka wakazi wa jimbo hilo kubadili mtazamo wao kwa kuwachagua viongozi wachapa kazi.

Akiwahutubia mamia ya wakazi  wa Bunda  juzi katika mkutano wa hadhara mjini Bunda, mjumbe wa mkutano mkuu wa wa taifa CHADEMA Bw. Godbless Lema alisema kuwa matatizo ya watu wa Bunda kamwe hazitaisha kama hawatafanya uamuzi wa kuachana  na Wasira.

Alieleza baadhi ya mapungufu ya Wasira ni pamoja na uzee hali inayomsababisha kuzinzia bungeni kutokana na kushindwa kustahimili hoja ngumu zinazoibuliwa na wabunge vijana.

“Huyu Wasira kila anapoingia Bungeni ni usingizi tu, katu hawezi kubadilisha Bunda, ni Mzee wa usingizi” alisema Lema a kuongezea.

“Watu wa Bunda mlifanya makosa kuwa na mbunge mchapa usingizi bungeni…msisubiri malaika awaondolee usingizi wenu, wapeni CHADEMA nafasi  ili kutafuta uhuru na haki mliopoteza kwa muda mrefu”.
“achaneni na huyu mzee mchapa usingizi, hatuko tayari kubishana naye kwenye jukwaa” alisema Lema.

Kuhusu  kero la maji linalowasumbua wakazi wa mji wa Bunda, Lema alidai licha ya fedha nyingi zinazotolewa na serikali kwa maendeleo ya maji mjini Bunda  bado Wasira ameshindwa kukidhi mahitaji ya maji.
“maji yako umbali wa kilomita 12 tu lakini watu wa Bunda hawana maji kwa sababu ya ufisadi unaofanywa na viongozi wa serikali” alisema Lema.

Aidha aliwaadharisha wananchi  na kuwataka waishinikize serikali kushughulikia ufisadi wa viongozi kutorosha fedha za umma katika benki za nchi ya Uswisi wakati wao wanakosa huduma bora za jamii.

Naye mratibu wa kampeni hiyo inayojulikana kama ondoa CCM Bunda  Bw.Lucas Webiro alionesha kukerwa na hali ya upungufu wa madawa  ambapo madaktari baada kuwapima wagonjwa uwape cheti na kuwalekeza katika maduka yao.

Alihoji wakopata  dawa madaktari hao wakati serikali inadai kukosa huku akikerwa na hali ya rushwa ilikithiri katika utoaji wa huduma.

Webiro aliwataka wananchi na viongozi kurudia  maadili ya Baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.  

Wakati huo huo  mtalo wa kutandaza mabomba  katika mradi mkubwa wa maji mjini  inayofadhiliwa na benki kuu ya dunia kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania umefukiwa kwa madai kuwa ulikosewa ramani.

Baadhi ya watalaamu wa maji katika halmshauri ya wilaya ya Bunda wamedai kuwa mtalo huo uliochimbwa upande wa kushoto mwa barabara ya kutoka Bunda-Ukerewe ulikosewa ramani na sasa utachimbwa upande wa kulia.

Mtalo huo ulioanza katika chanzo cha maji ya Nyabehu  hadi  katika Kijiji cha Migungani wastani wa kilomita  10 uliokuwa ukijengwa na kampuni ya Nyakirang’anyi Contruction umefukiwa.

Hapo awali wakati  mitalo hiyo ikichimbwa Mbunge wa jimbo la Bunda Stephen Wasira aliambatana na waandishi wa habari hadi katika eneo hilo ambapo waandishi walishuhudia mitambo ikiendelea na kazi ya kuchimba mitalo na kuonesha ufanisi mzuri hali ambayo sasa ni tofauti  baada ya miezi michache.

Hivi karibuni baadhi ya waandishi wa habari  walitembelea eneo hilo na kukuta  kazi imesimama huku mitalo kiwa imefukiwa .

Mradi huo wa maji unakadiriwa kugharimu zaidi ya sh.20 bilioni  ulianza kutekelezwa mwaka 2007 ambapo kwa mujibu wa wasimamizi wa mradi huo ambao ni mamlaka wa maji safi na taka mjini Musoma(MUWASA) ungekamilika mwaka 2010.

Kwa Mujibu wa Meneja wa  mamlaka wa maji mjini Bunda Iddi Swai hadi sasa hatua ilifikiwa ni ujenzi wa matanki ya maji, ununuzi wa pampu, uchimbaji wa mitalo ya kulazia mabomba, mpango wa kujenga chujio katika chanzo cha maji Nyabehu katika ziwa Victoria na hatua ya TANESCO ya kuweka umeme.


Alidai kuchelewa kukamilika kwa mradi huo ni kutokana na vigezo vya kimataifa vilivyotolewa na Benki kuu ambavyo vilitakiwa vikamilishwe na Wizara ya maji kabla ya mradi huo kuanza ikiwa ni pamoja na ramani ya mradi.Chanzo Pasco Michael

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE