CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE TANZANIA TAMWA KIMETOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA KUANDIKA NA HABARI ZA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO
Mkurugenzi wa Chama Cha waandishi wa habari wanawake( TAMWA) Bi Valerie Msoka |
Nikielekea Ukumbini kwa ajili ya kuanza mafunzo rasmi GoldLand Hotel |
Niko na Dj Cares one kwenye samaaaaaki samaki |
Mimi na Rejina toka Sachita Fm Tarime |
Eneo la Bustani Goldland Hotel |
Baada ya mafunzo kilichofuata nia kupiga picha katika madhali ya GoldLand hotel Tarime |
Waandishi wa habari wakisikiliza kwa makini katika mafunzo wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mkoani Mara |
Waandishi wa
habari mkoani Mara wamekishukuru Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake(TAMWA)
Kwa kuandaa mafunzo ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kwa waandishi
wa habari Mkoani Mara.
Wakitoa
shukrani zao kwa mkurugenzi mtendaji wa chama cha waandishi wa habari wanawake
Bi Valerie Msoka wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku mbili juu ya kuandika na
kuripoti habari za ukatili wa kijinsia wamesema kuwa chama hicho kinastahili
kupongezwa na kuwa mfano wa kuigwa kwa kutambua mchango wa waandishi wa habari
mikoani.
Wamesema
kuwa chama hicho ni mfano wa kuigwa na Taasisi na mashirika mengine kwa
kuwatumia waandishi wa habari wa eneo husika katika kuandika na kulipoti habari
wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto mkoani mara na sio kuwatumia
waandishi wa habari toka dar es salaam wakati waandishi wa mikoani wapo.
Katika
mafunzo hayo ambayo mgeni rasimi alikua mkuu wa wilaya ya Tarime John Enjewele
yamewapa mbinu za kuandika habari za ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Wamesema
changamoto kubwa inayowakabili katika kuandika habari za ukatili fedha kwa ajili ya kusafiri sehemu moja hadi
nyingine kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili kuandika makala na vipindi vya
redio na televisheni.
Kwa mujibu
wa tafifiti mbalimbali kuhusu ukatili wa kijinsia kwa wanakwake na watoto mkoa
wa Mara ni miongoni mwa mikoa hapa nchini ambayo inafanya vitendo vya ukatili
wa kijinsia kwa asilimia 72 Hivyo wameamua kuandaa mafunzo hayo kwa waandishi
ili wasaidie kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
kwa waandishi kutoa elimu kwa jamii na kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia
kwa wanawake .
Mafunzo hayo
yalifanyika wilayani tarime katika ukumbi wa GoldLand hotel kuanzia tarehe
3-4/12/2012.
Comments
Post a Comment