Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Asalom Mwakyoma
Mtu  mmoja  asiyefahamika majina amekutwa amekufa huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwa na panga  katika kijiji cha magunga kata ya buhemba wilayani butiama mkoani mara

Kamanda wa polisi wa mkoa wa mara ,kamishina msaidizi Absalom Mwakyoma amethibitisha tukio hilo ambapo jeshi hilo linafanya uchunguzi ili kubaini marehemu huyo kuwa ni mkazi wa wapi,ambapo mwili wake umeletwa kuhifadhiwa katika chumba cha maiti musoma.

Wakati huo usiku wa kuamkia leo watu wasiofahamika  wamevamia nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo kwa jina la yote heri iliyoko buhemba wakiwa na silaha aina ya smg huku wakijitambulisha kuwa ni askari polisi  na kuwaamuru wateja wote kufungua milango na kuwapora  simu na fedha na baada ya kutekeleza wizi huo watu hao walitokomea kusikojulikana.

Jeshi la polisi mkoani mara linaendelea kuwasaka majambazi hayo ambapo pia limewaomba wananchi kutoa ushirikiano katika kuwasaka watuhumiwa.
  
Huko wilayani bunda askari wa jeshi la polisi na familia zao wilayani Bunda mkoani Mara wameingia katika adha kubwa ya kulazimika kutumia  tochi, vibatari na mishumaa kwa kukosa umeme takriban mwezi mmoja sasa.

Hatua hiyo imekuja kutokana na taasisi hiyo kushindwa kununua luku za umeme kwa matumizi ya ofisi  na katika makazi ya askari hao.

Kwa sharti ya kutotajwa majina baadhi ya askari hao jana wamewaeleza waandishi wa habari waliofika kituoni kujionea hali kuwa umeme unaotumika katika kituo hicho  hulipwa na baadhi ya viongozi wa kituo kwa kujitolea.

Walisema katika makazi yao hali ni mbaya zaidi kutokana na serikali kutowapelekea fedha za kununua umeme.

“ tunaishi maisha ya shida sana maana kama kambi ya polisi wanaolinda usalama wa raia tunakosa umeme ni hatari  hata kwa usalama wetu” alisema askari mmoja.

Meneja wa Tanesco wilaya ya Bunda Sosthenes  Lushamisa alidai kuwa  tatizo la polisi kutokuwa na umeme ni lao wenyewe kutokana na kutonunua LUKU katika  mita ya TANESCO waliyofungiwa katika kambi yao.

Bw. Lushamisa alifafanua kuwa askari hao wana matumizi makubwa ya umeme lakini wanashindwa kununua umeme wa kutosha na kwa wakati.

Alidai Shirika lake halina tatizo labda la kiufundi jambo ambalo bado hawajapata malalamiko yoyote kutoka polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mara Absalum Mwakyoma alipoulizwa kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi alidai kuwa hana taarifa zozote za polisi Bunda kukosa umeme huku akiahidi kufuatilia.

Wananchi wanaoishi karibu na kambi hiyo wamesikitishwa na kambi la polisi kukaa gizani jambo ambalo ni hatari kwa ulinzi na usalama na kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS