KARUME STADIUM SERENGETI FIESTA MUSOMA BHAAAAS!

Tamasha la Serengeti Fiesta ndani ya musoma Linatarajia kufanyika kesho siku ya ijumaa ndani ya uwanja wa karume kuanzia saa 12 kamili jioni.

Tamasha hilo linaloratibiwa na kampuni ya Prime Time Promotion ya jijini dar es salaam linafanyika kila mwaka katika mikoa tofauti hapa nchini Tanzania kwa kuwashirikisha wasanii wa ndani nje ya nchi kwa lengo la kutoa burudani na kuelimisha jamii husani vijana juu ya mambo mbalimbali.

Wakiongea na blog hii kwa nyakati tofauti vijana wa musoma wamesema wanasema wanasubiria kwa hamu kuona baadhi ya wanasinii kama vila Ney wa Mitego, Bi Cheka, Mh temba na wengine wengi ambao wanafanya vizuri sana katika anga ya muziki wa bongo Fleva.

Kingilio katika tamasha hilo ni shilingi Elfu tano  huku Kinywaji cha Bia ya Serengeti Lager na vinywaji vya kampuni hiyo ndio vitauzwa ndani ya uwanja huo wakiwa ndio wadhamini wakuu wa tamasha hilo.

Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta

TOZI GAMBA AFUNIKA SHOW YAKE NA THE TRACK MASTERS DJS BWALO LA POLISI MWISENGE SIKU YA CHRISTMAS