C-sir Madini Kuachia ngoma Mwezi ujao

Msanii wa Miondoko ya Mziki wa kizazi kipya C-Sir Madini kutoka Mwenye maskani yake Jijini mwanza mwezi ujao anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Pain Killer.

Madini amesema kuwa wimmbo huo tayari umekwisha kamilika na amerekodi katika studio za tetemesha record chini ya mtayarishaji wake Kid Bwoy ambae ndie mtayarishaji wake toka anaanza kuimba jijini mwanza.

Amesema kwa sasa studio za tetemesha ziko jijini dar es salaam ambapo amesema mashabiki wake wakae tayari kuupokea wimbo huo ambao hivi sasa amekamilisha kurekodi video yake chini ya Adam Juma wa Next level.

C-Sir madini ni moja ya wasanii wanaofanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya toka mwanza aambo wamesaidiwa kwa kiasi kikubwa na mmiliki na mtayarishaji wa studio ya tetemesha kurekodi nyimbo kali akiwa na wasanii wengine ni Hussein Machozi, Sajna na wengine wengi.

Wasanii wengine wanaotokea mwanza ambao wanafanya vizuri katika mziki wa bongo Fleva ni pamoja na H-Baba, Fid Q pamoja na hardmard

C-Sir Madini akiwa na Joketi wakiwa katika maandalizi ya kurekodi wimbo wa wa Pain Killer: Picha kwa hissani ya Djchoka  


Comments

Popular posts from this blog

KATI YA KUKU NA YAI KIPI KILITANGULIA?

NGUO ZA NDANI ZINAZOBANA KWA WANAUME ZINAATHIRI UWEZO WA MBEGU ZA KIUME KUWEZA KUTUNGA MIMBA

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE