Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma ipo njia panda kwenda kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta
Timu ya wachezaji watumishi wa manispaa ya musoma huenda ikashindwa kushiriki katika mashindano ya shirikisho la michezo serikali za mitaa Tanzania Shimisemta, baada ya wachezaji wa timu hiyo kudai kuwa hajapewa fedha toka katika ofisi ya mkurugenzi kwa ajili ya kwenda kushiriki katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika huko morogoro. Wakiongea kwa sharti la kutotajwa majina yao baadhi ya watumishi hao wamesema japokuwa wamekuwa wakitenga muda wao kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo lakini wanashindwa kufanya mazoezi kwa uhakika kutokana na mkurugenzi wa manispaa ya musoma mpaka kutowathibitishia kwenda kushiriki katika mashindano huku zikiwa zimebaki siku nne mashindano hayo kuanza. Wachezaji hao wamedai kuwa wanashindwa kuelewa toka mwaka 2000 timu ya watumishi wa manispaa ya musoma haijashiriki katika mashindano hayo kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti lakini timu za manispaa ya Musoma vijijini, Bunda, Serengeti pamoja na Tarime zim