Posts

Showing posts from December, 2023

SERIKALI YAJIPANGA KUONGEZA VIRUTUBISHO KWENYE VYAKULA KUONDOA TATIZO LA WATOTO VICHWA VIKUBWA.

Image
  Na Lubango Mleka-Dodoma Katika kuhakikisha matatizo ya ukosefu wa lishe unaowakabili binadamu wakiwemo mama wajawazito ambao upelekea kuzaa watoto wa vichwa vikubwa na mgongo wazi unatoweka ,Serikali imejipanga kuongeza virutubisho vya vitamini na madini kwenye vyakula ambavyo vitasadia kuimarisha kinga ya mwili.. Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Mtafiti na mratibu wa shughuli za uongezaji virutubishi kitaifa , Selestine Mgoba wakati alipokuwa kwenye warsha ya kutekeleza maagizo ya viongozi juu ya kupambana na upungufu wa lishe iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na kuwakutanisha wanakamati kutoka wizara mbalimbali na Sekta binafsi. Amesema kuwa kutokana na matatizo hayo wamechagua vyakula vikuu ambavyo ni unga wa ngano,unga wa mahindi,mafuta ya kula na chumvi ambavyo vitaongezwa madini ya chuma ambavyo vitaimarisha kinga ya mwili na kwa akina mama kuwa msaada. "Tunaona kwenye Taifa letu upungufu wa Damu ambayo usababishwa na upungufu wa madini chumvi zaidi y