Posts

Showing posts from January, 2013

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA SILKONI KUONGEZA MAKALIO KWA WANAWAKE

Image
Madhara ya Dawa za Kuongeza Makalio NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo. Taarifa hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu za nyuma (chini) baada ya muda mfupi. Imebainika kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya ya binadamu. Wataalamu wa mambo wanadai kwamba pamoja na kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi ya makalio katika mpangilio usio sahihi. Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa  saratani. Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke ali

WATU WAWILI WAZIKWA KATIKA KABURI MOJA WAKIWA HAI HUKO MKOANI MBEYA

Image
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani WAKAZI wawili wa Kijiji cha Karungu, Kata ya Ivuna, Wilaya ya Momba, mkoani Mbeya wamefariki dunia baada ya kufukiwa wakiwa hai katika kaburi moja na marehemu wanaodaiwa kumuua, tukio linalohusishwa na imani za kishirikina. Watu hao, Ernest Molela anayekadiriwa kuwa na umri zaidi ya miaka 60 na Bibi Mizinala Nachela ambaye umri wake unakadiriwa kuwa zaidi ya miaka 50, walizikwa wakiwa hai pamoja na aliyekuwa mkazi wa kijiji hicho, marehemu Nongwa Hussein. Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ivuna, Joseph Silwimba aliliambia gazeti hili jana kwa simu kuwa, tukio hilo lilitokea juzi kati ya saa tano na sita mchana, muda mfupi kabla ya maziko ya Hussein. Kabla ya kufukiwa katika kaburi moja na marehemu, Molela na Nachela kwa nyakati tofauti walipigwa hadi kuzirai na watu wanaodaiwa kushiriki kuchimba kaburi kwa ajili ya kumzika marehemu Hussein. Silwimba alisema Hussein alifariki dunia Jumamosi saa 10 jioni baada ya kuu

AMCHOMA MKE WAKE SEHEMU ZA SIRI NA CHUMA CHA MOTO KUTOKANA NA WA MAPENZI

MWANAMKE mkazi wa Kijiji cha Matui, wilayani Kiteto, mkoani Manyara ameponea chupuchupu kuuawa baada ya mume wake kumchoma na chuma cha moto sehemu za siri kutokana na wivu wa mapenzi. Mwanamke huyo alifanyiwa kitendo hicho juzi usiku kwenye kijiji hicho, baada ya mume wake  kumtuhumu kuwa ana uhusiano wa mapenzi na msaidizi wao wa nyumbani. Akizungumza kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kiteto juzi, wakati akipatiwa matibabu mwanamke huyo alisema hivi sasa anasikia maumivu makali. Alisema alipofanyiwa kitendo hicho alipoteza fahamu kwa muda mrefu, kwani alitokwa na damu nyingi na alizinduka baada ya kufikishwa hospitalini hapo iliyopo umbali wa kilomita 32 kutoka nyumbani kwake.   Aliongeza kuwa kabla ya kufanyiwa kitendo hicho, kila mara mume wake alikuwa anamweleza kuwa amesikia tetesi kuwa ana uhusiano wa mapenzi na msaidizi wa kazi, hivyo atamfanyia kitu ambacho hatakisahau. “Siku ya tukio hilo alikoka moto akachukua nondo ya kuweka alama kwenye ng’ombe,  akan

NGONO INASABABISHA SARATANI YA KIZAZI

Image
UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa saratani ya shingo ya kizazi, inasababishwa pamoja na mambo mengine na ngono kama ilivyo kwa ugonjwa wa Ukimwi, madaktari bingwa wa magonjwa ya maradhi hayo wamesema. Hayo yalielezwa na daktari bingwa wa uchunguzi wa magonjwa katika Kitengo cha Patholojia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Henry Mwakyoma na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Saratani katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Crispin Kahesa. Madaktari hao wametaja mambo mengine yanayoweza kusababisha saratani ya shingo ya kizazi kuwa ni kujiingiza kwenye mapenzi katika umri mdogo, kuolewa mara nyingi, kuwa na wapenzi wengi, kusafisha sehemu za siri kwa bidhaa zenye kemikali na kuzaa mara nyingi. Katika kiwango cha kimataifa, wastani wa mwanamke kuzaa bila kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa saratani, ni watoto wanne. Dk Mwakyoma alisema saratani ya shingo ya kizazi inatokana na aina 40 ya virusi, aina mbili ikiwa ni virusi vinavyosambaa kwa njia ya

THE TRACK MASTERS DJs NDIO HABARI YA MJINI PALE BWALO LA POLISI MWISENGE

Image
Kadri muda ulivyozidi kwenda ndio ze nyomi inazidi kuongezeka tunawashukuru sana Watu wakazidi kuongezeka watoto kwa wakubwa Jioni watu walianza kuja mapema kusherekea mwaka mpya bwalo la polisi mwisenge