Fahamu Jinsi Wavuvi wa Mwalo wa Kayenze Ndogo ilemela Mwanza Wanavyotumia Solar Kukausha Dagaa Kwa Kutumia Solar Dryer
Na Emmanuel Chibasa Katika mwalo wa Kayenze ndogo, wilaya ya Ilemela, jijini Mwanza, wavuvi na wafanyabiashara wa dagaa sasa wanashuhudia mabadiliko makubwa kupitia teknolojia ya kisasa ya nishati ya jua, inayotumika kukausha dagaa. Mradi huu, unaoendeshwa na kampuni ya Millennium Engineers, umeleta matumaini mapya kwa sekta ya uvuvi kwa kuwawezesha wavuvi kukausha dagaa kwa ubora unaokidhi viwango vya soko la ndani na nje ya nchi. Kwa Nini Teknolojia Hii ni Muhimu? Teknolojia mpya ya ukaushaji dagaa kwa kutumia mitambo ya nishati ya jua ni muhimu kutokana na kutajwa kuwa suluhisho la kukabiliana na changamoto ya upotevu na uchakataji wa dagaa zenye ubora na hivyo kuongeza tija kwa wavuvi na wachuuzi katika ziwa victoria. Wavuvi na wafanyabiashara ya dagaa wanasema, Kabla ya mradi huo, wailikua wakianika dagaa kwenye mchanga au kwenye vichanja vya miti kando ya ziwa Victoria na njia hizi za jadi zilikuwa na changamoto kadhaa, zikiwemo kuathiri usafi wa dagaa, kuvutia uchafu na wadudu