Ni jambo la kawaida kwa watanzania kutojua umuhimu wa bajeti katika maisha yetu ya kila siku, na tunashindwa kujioji kama mapato yetu yanaendana na matumizi hata katika ngazi ya kaya au familia au mtu mmoja mmoja. Katika hali ya kawaida tumekuwa na matumizi makubwa kuliko kipato tunachokipata na hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi hawazingatii bajeti wanafikiri bajeti ni kwa ajili ya serikali, makampuni na taasisi wakisahau kuwa mtu anaweza kujiwekea bajeti katika maisha yao ya kila siku. Leo katika ujasiliamali nahitaji ufahamu kuna umuhimu gani wa kutengeneza bajeti kuanzia ngazi ya mtu, kaya au familia, makampuni makubwa, serikali pamoja na taasisi. Bajeti: Ni mpango unaonyesha kiasi cha pesa, rasilimali kinachopangiliwa kwa ajili ya kutumika.Kuna aina mbalimbali za bajeti ambazo zinatofautiana kwa tafasiri na utekelezaji. Ili mtu au taasisi pamoja na serikali iweze kufanikiwa katika maisha ni lazima kutengeneza na kufuata kanuni na kuzingatia mipango utakayoainisha ka...
Comments
Post a Comment