Posts

AJALI MBAYA ALIYOIPATA NDUGU YANGU DOMMY MKONO JUMAPILI 10/11/2013 MAGU

Image
BAADA YA AJALI GARI LIKIREKEBISHWA KWA AJILI YA KUVUTWA KULETWA MUSOMA SEHEMU YA KUSHOTO YA MUONEKANO BAADA YA AJALI AJALI ILIKUA MBAYA SANA KAMA UNAVYOONA YANI NI KUMUOMBA TU MUNGU SEHEMU YA MBELE YA GARI HILI IMEHARIBIKA VIBAYA HILI GARI LILILOKUA LIMEPAKI NA KUSABABISHA AJALI  MAENEO YA MAGU WATU WA USALAMA WAKIPIMA ANGALIA HUO MSTARI UNAONYESHA BREAK ALIZOZOSHIKA DOMI MPAKA ALIPOLIFIKIA ROLI HAPO KWA TRAFIKI WA KIKE. BAADA YA AJALI KUTOKEA HILI ROLI LILISOGEZWA PEMBENI KABISA YA BARABARA ILI MAGARI MENGINE YAWEZE KUPITA VIZURI BAADA YA KUMALIZA TARATIBU ZOTE  KATIKA KITUO CHA POLISI MAGU ILIFUATA KAZI YA KULIVUTA GARI HILI KULILETA MJINI MUSOMA NA HII ILIKUA JUMATATU 11/11/2013 SAA 11:16 JION SEHEMU YA NDANI MBELE PIA ILIHARIBIKA VIBAYA KAMA INAVYOONEKANA BAADA YA AJALI

VIWANGO VYA ALAMA YA MWANAFUNZI NA UFAULU

                                   JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA                                 WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU UTANGULIZI Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama  CA ) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi. Maoni ya wadau yamekusanywa kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika na utaratibu wake kat...

KABURI LA MTOTO ALIYEFARIKI MIAKA MITATU ILIYOPITA LAFUKULIWA BAADA YA KUONEKANA YUKO HAI

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kaburi ambalo alizikwa mtoto Shabani Maulidi (15), ambaye anadaiwa kufariki dunia miaka mitatu iliyopita na kuonekana akiwa hai hivi karibuni, jana lilifukuliwa na viungo vya mwili wake kukutwa ndani. Kazi hiyo iliyofanyika chini ya ulinzi mkali wa polisi pamoja na Mtafiti wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mwanza, Lucas Ndungulu, ilizua taharuki kwa umati wa watu waliokuwa eneo hilo, baada ya nyumba ya jirani lilipo kaburi hilo, Masanja Marwa, kubomoka ghafla wakati ufukuaji huo ukiendelea, huku mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja naye akianguka na kuzirai. Kwa sasa mtoto huyo ambaye alionekana hai, amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita kwa uangalizi wa kitaalamu. Akizungumza na waandishi wa habari eneo la tukio, Ndungulu alisema kuwa wameamua kufukua kaburi hilo ili kupata sehemu ya viungo vya mwili kwa ajili ya vipimo. “Lengo la kufukua kaburi hili ni kutaka tupate kiungo chochote cha ...

WATAKAO FELI MTIHANI WA KIDATO CHA PILI KURUDIA DARASA

Image
Wanafunzi Wakati wanafunzi wa kidato cha pili wakitarajia kufanya mtihani wa taifa wiki ijayo, Serikali imesema watakao feli watarudia darasa hilo. Kauli hiyo imetolewa na katibu mkuu wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi profesa Sifuni Mchome alipokua akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam. Alisema jumla ya wanafunzi 531, 457 wa kidato cha pili wanatarajia kufanya mtihani huo nchi nzima. “ watakao feli watarudia darasa hilo na watakao feli mara ya pili serikali itaangalia uwezekano wa kuwapeleka shule za ufundi au kuendelea na shule kama wanafunzi wa kujitegemea” alisema Profesa sifuni. Alisema mtihani huo utaanza October 7 hadi 21 mwaka huu katika vituo takribani 4,437 vilivyosajiliwa kwa ajili ya kufanyia mitihani nchi nzima na wanafunzi waliojiandikisha kufanya mitihani hiyo wasichana ni 270,734 sawa na asilimia 50.1 na wavulana ni 260,723 sawa na asilimia 49.1 ambao ni sawa na ongezeko la asilimia 3.1 ikilinganishwa na watahiniwa wa mwaka jana ...

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEMFUKUZA KAZI ASKARI ALIYEINGIA UKUMBI WA DISCO AKIWA NA BUNDUKI

KAMANDA wa Polisi Kikosi cha Operesheni ya kuwaondoa wahamiaji haramu na majambazi, maarufu kama Kimbunga, Simon Sirro, amesema kuwa wamemtimua askari wao aliyeingia ukumbi wa disko mjini Bukoba akiwa na bunduki kwa ajili ya kulipa kisasi. Sirro alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jana wakati akielezea mafanikio waliyoyapata katika operesheni hiyo kwa kuwakamata watuhumiwa 88 wanaojihusisha na ujambazi na biashara ya silaha. Alimtaja askari huyo kuwa ni mwenye namba H 85, PC Alphonce, aliyekuwa ametokea mkoani Mara kwa ajili ya kushiriki operesheni hiyo mkoani Kagera. Alisema kuwa PC Alphonce alikorofishana na baadhi ya watu ndani ya ukumbi wa disko, hivyo akatoka nje kufuata bunduki, kisha akarudi nayo kwa ajili ya kuwadhuru ‘wabaya’ wake, lakini askari wenzake waliokuwamo ndani walifanikiwa kumzuia kabla ya kutimiza azima yake. Kuhusu kukamatwa kwa Mkurugenzi wa redio ya kijamii iliyoko wilayani Karagwe (FADECCO) na kuwekwa ndani siku mbili, kis...

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA AFANYA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA MARA KUBORESHA MAHUSIANO

Wito umetolewa kwa wanasiasa na wanachama wa chama cha mapinduzi Mkoani Mara kuacha Siasa za makundi ndani ya chama ili kukimalisha na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) Mkoani Mara Bwana Christopher Mwita Sanya, alipokua akijibu maswali mbalimbali toka kwa Waandishi wa Habari Mkoani Mara katika ofisi za chama hicho zilizopo mtaa wa nyasho mjini Musoma. Sanya amesema siasa za makundi hazitakiwi kwani zinarudisha nyuma maendeleo ya chama na Taifa kwa ujumla na tayari chama hicho kimeanza vikao vyenye lengo la kuondoa makundi na kuboresha utendaji kazi wa chama hicho. Amesema chama hicho kimejiwekea utaratibu wa kuwakumbusha madiwani na wabunge wa chama hicho kutekeleza ahadi wanazotoa kwa wananchi ili kurejesha imani kwa wananchi kuwa ahadi wanazotoa katika chaguzi mbalimbali wanazitekeleza. Mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi mkoani mara leo amefanya kikao hicho na waandishi wa habari kwa len...

MUDA WA KUBADILISHA LESENI SASA MWISHO APRIL 31

Matatizo ya kukatika kwa umeme ni miongoni mwa sababu zilizosababisha polisi nchini na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulazimika kuongeza muda wa utoaji wa leseni mpya hadi Aprili 31 mwaka huu badala ya Machi 31 iliyopangwa. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema wamelazimika kuongeza siku baada ya kubaini kuwapo kwa mambo kadhaa yaliyokwaza baadhi ya madereva kubadilisha leseni zao kama inavyotakiwa. “Tumebaini madereva hao walishindwa kubadili leseni zao kutokana na kukosekana kwa mtandao ambao ndiyo unawezesha mawasiliano ya kielektroniki kati ya TRA na trafiki, ingawa pia siku za kazi ziliingiliana na Sikukuu ya Pasaka’’ alisema. Alisema baadhi ya madereva wengine nao  hawajamaliza mafunzo yao ya PSV katika Vyuo vya NIT na Veta huku wengine wakichelewa kupewa vyeti vyao licha ya kumaliza mafunzo hayo,”alisema Mpinga. Alisema kutokana na sababu hizo wameamua kuongeza muda ikiwa n...